Mashirika na viwanda vya kiserikali vya China vyasaidia zaidi Mkoa wa Xinjiang katika kuongeza nafasi za ajira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2024

Picha hii iliyopigwa Novemba 15, 2023 ikionyesha Kisima cha Yuejin 3-3XC cha Shirika la Petroli la China (Sinopec) katika Bonde la Tarim, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Xiao Yijiu)

Picha hii iliyopigwa Novemba 15, 2023 ikionyesha Kisima cha Yuejin 3-3XC cha Shirika la Petroli la China (Sinopec) katika Bonde la Tarim, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Xiao Yijiu)

BEIJING - Mashirika na viwanda vya kiserikali yanayosimamiwa na serikali kuu ya China (SOEs) yameongeza juhudi za kusaidia Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang katika kuongeza nafasi za ajira tangu Mwaka 2022, yakiahidi kusaidia zaidi maendeleo yenye sifa bora ya juu mkoani Xinjiang.

Serikali ya Mkoa wa Xinjiang na Mamlaka ya China ya Udhibiti na Usimamizi wa Mali ya Kitaifa zilifanya mkutano siku ya Jumatatu, mkutano huo umesema, kazi za mashirika na viwanda vya kiserikali katika kusaidia maendeleo ya mkoa huo imepata matokeo dhahiri katika miaka miwili iliyopita.

Miradi jumla ya 227, inayoungwa mkono na mashirika na viwanda hivyo 41, imepanga uwekezaji wenye thamani ya jumla ya yuan trilioni 1.1 (kama dola bilioni 155 za Marekani)

Uwekezaji huo unahusisha sekta mbalimbali, zikiwemo mafuta ya petroli, gesi asilia, makaa ya mawe, nishati mpya, uchukuzi, ulinzi wa mazingira, mawasiliano, afya na ujenzi wa miundombinu. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, juhudi hizi zimetoa nafasi za ajira kwa watu takriban 251,000 kwa jumla, amesema Chen Weijun, naibu mwenyekiti wa serikali ya mkoa wa Xinjiang.

Kwa kuunganisha nguvu bora za viwanda vya kiserikali na hali halisi ya Xinjiang, mashirika na viwadna vilivyohudhuria kwenye mkutano huo vimepanga mipango ya kusaidia viwanda vya Xinjiang kati ya 2024 na 2026. Katika kipindi cha miaka mitatu, vinatakiwa kuwekeza katika miradi 133 yenye thamani ya jumla ya karibu Yuan bilioni 695, na inapanga kuajiri wafanyakazi wapya 33,000.

Zhang Yuzhuo, mkurugenzi wa Kamati ya Udhibiti na Usimamizi wa Mali ya Kitaifa ya Baraza la Serikali la China, amesema kuwa ili kusaidia maendeleo ya Xinjiang, mashirika na viwanda hivyo vitaboresha zaidi ushirikiano wa kiviwanda, kuongeza uwekezaji katika teknolojia ya hali ya juu, sekta mpya na masoko yanayoibukia, kuendeleza nguvukazi mpya zenye sifa bora, na kuongeza uwezo wa kutoa nafasi za ajira kwa kupitia maendeleo ya viwanda mkoani Xinjiang. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha