

Lugha Nyingine
Ushirikiano wa kilimo na China waleta ajira, maendeleo endelevu zaidi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Guismala-Hamza, waziri wa kilimo na maendeleo ya vijijini wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Bangui, CAR, Februari 7, 2024. (Xinhua/Han Xu)
BANGUI - Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imeshuhudia mafanikio makubwa katika kilimo kutokana na ushirikiano wake na China, Guismala-Hamza, waziri wa kilimo na maendeleo ya vijijini wa CAR, amesema katika mahojiano ya hivi karibuni huku akiongeza kuwa miradi mikubwa ya kilimo ya China siyo tu inatoa mahitaji ya kimsingi na ajira lakini pia fursa mpya za mafunzo na ujuzi kwa watu wa CAR.
"Miradi hii imeleta manufaa kwa nchi, kwanza katika sekta ya uchumi, na pia yanapunguza umaskini kutokana na kutoa ajira kwa vijana," Guismala-Hamza amesema.
Miradi ya maendeleo ya China kwa kawaida inatafuta "kuiondoa Afrika kutoka katika taabu, umaskini," Guismala-Hamza amesema, huku akibainisha kuwa Juncao, teknolojia iliyoanzishwa na China kwa kutumia nyasi kukuza uyoga, inashikilia ufunguo wa kupata mustakabali mzuri wa wakulima wadogo nchini humo.
Teknolojia ya Juncao, iliyoanzishwa na Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian nchini China, tangu Mwaka 2021 imewezesha wakulima wadogo nchini CAR kupanda uyoga kutoka kwenye nyasi zilizokaushwa na kukatwa, bila kukata miti na kuharibu mazingira.
"Mradi wa Juncao ni mradi mzuri sana, ambao umewasisimua wakazi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa sababu ya urahisi wake. Mafundi wa China walitoa mchango mkubwa sana (katika kutekeleza mradi huo). Mafundi wengi walipatiwa mafunzo nchini China, na leo kuna mafundi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wanatumia teknolojia hii,” amesema, huku akisema kuwa CAR inajadiliana na China kwa ajili ya awamu ya pili ya mradi huo ambayo italenga zaidi maeneo ya vijijini.
Kwa mujibu wa Guismala-Hamza, CAR inafanya kazi ya kukifanya kilimo chake kuwa cha kisasa na inategemea uzoefu, ujuzi wa kiufundi na mtindo wa China katika sekta ya kilimo cha chakula kwa ajili ya utekelezaji mzuri.
"Kwa kweli China iko katika nafasi nzuri ya kutusaidia kwa mashine za usindikaji," afisa huyo amesema, huku akiongeza kuwa CAR ina aina mbalimbali za bidhaa za kilimo, ikiwa ni pamoja na kahawa, pamba na miwa, ambazo zinaweza kuvutia washirika wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma