

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China asisitiza mafungamano ya kina ya Uvumbuzi wa teknolojia na uvumbuzi wa viwanda
Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alipofanya ukaguzi mjini Beijing alitembelea Taasisi ya Teknolojia za Akili Mnemba ya Beijing. Machi 13, 2024. (Xinhua /Liu Bin)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang alipofanya ukaguzi mjini Beijing siku ya Jumatano alitoa wito wa kuendeleza kazi ya mafungamano ya kina uvumbuzi wa teknolojia na uvumbuzi wa viwanda, na kuharakisha kuandaa msukumo mpya na nguvu bora mpya kwa ajili ya maendeleo yenye ubora wa hali ya juu.
Wakati wa ukaguzi wake kwenye kituo cha uendeshaji cha eneo la kielelezo la magari ya kujiendesha kiotomatiki kwa kiwango cha juu mjini Beijing, Waziri Mkuu Li ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amehimiza kuimarishwa kwa uungaji mkono katika utungaji wa vigezo na kuhakikisha kazi muhimu zinazohusika, ili kuhimiza maendeleo ya viwanda vya magari na ujenzi wa miji ya teknolojia za kisasa kwa kupitia uboreshaji wa teknolojia za kuendesha vyombo vya usafiri kiotomatiki.
Katika eneo la ofisi za Yizhuang za kampuni kubwa ya teknolojia ya China ya Baidu, Waziri Mkuu amesisitiza kwamba ni lazima kutumia nguvu bora za mazingira ya matumizi ya programu za kiteknolojia nchini China, kuongeza uungaji mkono wa taasisi, na kujenga mazingira yenye unyumbufu zaidi kwa ajili ya maendeleo ya viwanda vya teknolojia za akili mnemba.
Alipotembelea Kampuni ya Teknolojia ya Naura, Waziri Mkuu Li ameitia moyo kampuni hiyo kuongeza uwekezaji wa kiteknolojia, kuharakisha utafiti na uendelezaji wa bidhaa (R&D) kwenye vifaa vya kuchakata vyenye kutumia teknolojia ya hali ya juu, na kuhimiza uvumbuzi shirikishi katika mnyororo mzima wa viwanda.
Waziri Mkuu pia alikagua Taasisi ya Teknolojia za Akili Mnemba ya Beijing na kutoa wito wa kufikia mafanikio mapya kwa rasilimali na ushirikiano wa hali ya juu.
Baadaye aliongoza kongamano na kueleza kuwa kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora ni hitaji la kimsingi na lengo muhimu la kusukuma mbele maendeleo yenye ubora wa hali ya juu, huku akihimiza juhudi za kufikia mafanikio katika teknolojia ya msingi katika nyanja muhimu, na kuhimiza uvumbuzi wa viwanda kupitia uvumbuzi wa kiteknolojia ili kuharakisha kuanzisha mfumo wa viwanda vya kisasa ambavyo viwanda vya utengenezaji bidhaa kwa teknolojia ya hali ya juu vikiwa ni uti wa mgongo wake.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya ukaguzi katika Kampuni ya Kundi la Teknolojia la Naura mjini Beijing, China, Machi 13, 2024. (Xinhua/Liu Bin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma