Kutatuliwa mapema kwa hali ya mpaka kati ya China na India kunalingana na maslahi ya pamoja ya pande zote mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema siku ya Jumatano kuwa kutatuliwa mapema kwa hali ya mpaka kati ya China na India kunalingana na maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili China na India, na ameongeza kuwa kuna matumaini kuwa nchi hizo mbili zitapata suluhu kwa masuala husika ya mpaka ambayo inaweza kukubaliwa na pande zote mbili mapema iwezekanavyo.

Msemaji Wang ametoa maoni hayo kwenye mkutano na wanahabari kwa ajili ya kujibu habari kuhusu kauli ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar kuhusu hali ya sasa ya uhusiano kati ya India na China.

Nchi mbili China na India zote zinaamini kwamba kutatuliwa mapema kwa tatizo la hali kwenye mpaka kati ya China na India kunalingana na maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili, Wang amesema.

Amesema China inatumai kuwa pande hizo mbili zitafuata maoni ya pamoja ya viongozi wa nchi hizo mbili na kufuata misingi ya makubaliano husika, kudumisha mawasiliano kupitia njia za kidiplomasia na kijeshi, na kutafuta suluhu ya masuala husika ya mpaka ambayo inaweza kukubaliwa na pande zote mbili mapema iwezekanavyo.

China imesisitiza mara nyingi kwamba suala la mpaka haliwakilishi ukamilifu wa uhusiano kati ya China na India, na linapaswa kuliweka kwa kufaa kwenye uhusiano wa pande mbili na kudhibiti na kusimamia hali kwa mwafaka, Wang amesema.

China inatumai kuwa India na China zitafanya juhudi kwa mwelekeo sawasawa, kushughulikia uhusiano wa pande mbili kutoka mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, Wang amesema huku akiongeza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kuongeza hali ya kuaminiana na kuepuka kutoelewana na kuchukua maamuzi kwa makosa, kuzidisha mazungumzo na ushirikiano na kuepuka kuweka vizuizi, kushughulikia tofauti kwa mwafaka, na kuepuka kuzusha migogoro.

"Tukifanya hivyo, tutauwezesha uhusiano wa pande mbili ufuate njia ya kuendelea vizuri na kwa utulivu ," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha