Wabunge wa EU waidhinisha Sheria ya Teknolojia za Akili Mnemba (AI)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2024

Watu wakitembelea Kongamano la Kimataida la Simu (MWC) Mwaka 2024 mjini Barcelona, Hispania, Februari 26, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

Watu wakitembelea Kongamano la Kimataifa la Simu (MWC) Mwaka 2024 mjini Barcelona, Hispania, Februari 26, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

BRUSSELS - Bunge la Ulaya Jumatano limeidhinisha Sheria ya Teknolojia za Akili Mnemba (AI) kwa wingi wa kura mjini Strasbourg, Ufaransa ambapo sheria hiyo iliyopitishwa na wabunge 523 waliopiga kura ya ndiyo, 46 kura ya hapana na 49 wakijizuia kupiga kura ni mfumo kazi wa kwanza kabisa wa kisheria juu ya AI duniani, na imetumia mbinu inayozingatia hatari, ikiweka matumizi AI yenye hatari kubwa katika udhibiti mkali.

Kamishna wa Ulaya kwa Soko la Ndani Thierry Breton amekaribisha kupitishwa kwa sheria hiyo, akisema kuwa "Ulaya sasa ni mpangaji viwango wa kimataifa katika AI."

Chini ya sheria hiyo mpya, baadhi ya programu za AI zitapigwa marufuku, ikiwa ni pamoja na mifumo ya uainishaji wa kibayometriki wa kujikita katika sifa nyeti, na kuchukua picha za uso bila ya lengo kutoka kwenye mtandao wa intaneti au picha za CCTV kwa ajili ya kanzidata ya utambuzi wa uso.

Zaidi ya hayo, Sheria hiyo inakataza utambuzi wa hisia katika maeneo ya kazi na shuleni, alama za kijamii, kazi za polisi za kutabiri uharifu, na AI iliyoundwa ili kudhibiti tabia za binadamu au kutumia vibaya udhaifu wa binadamu.

Kwa mifumo ya madhumuni ya jumla ya AI (GPAI), Sheria hiyo inahitaji ufuataji wa mahitaji ya uwazi, kama vile kuzingatia sheria za hakimiliki za Umoja wa Ulaya (EU) na kuchapisha muhtasari wa kina wa maudhui yanayotumika kwa mafunzo.

Watu wakitembelea Kongamano la Kimataida la Simu (MWC) Mwaka 2024 mjini Barcelona, Hispania, Februari 28, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

Watu wakitembelea Kongamano la Kimataida la Simu (MWC) Mwaka 2024 mjini Barcelona, Hispania, Februari 28, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

Bird and Bird, Shirika la sheria la kimataifa, limebainisha kuwa mazungumzo yanayohusu Sheria hiyo ya AI yalileta masuala kadhaa yenye utata, hasa kuhusu mifumo ya AI ya utambuzi wa kibayometriki.

Kampuni hiyo imeangazia matatizo katika maandishi ya sheria hiyo ambayo yanaweza kuleta hali ya kutokuwa na uhakika ndani ya sekta hiyo, haswa kuhusu makatazo na vizuizi kwa utambuzi wa kibayometriki, pamoja na umaalum na tahadhari.

Sheria hiyo itaanza kutumika kikamilifu ndani ya miezi 24 baada ya kuanza kutumika. 

Mshiriki akipiga picha katika baraza lenye kaulimbiu isemayo "Mtandao wa Nguvu za Kompyuta: Mtandao Mahiri Zaidi kwa ajili ya Dunia Mahiri Zaidi" kwenye Kongamano la Kimataifa la Simu Mwaka 2024 mjini Barcelona, Hispania, Februari 27, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

Mshiriki akipiga picha katika baraza lenye kaulimbiu isemayo "Mtandao wa Nguvu za Kompyuta: Mtandao Mahiri Zaidi kwa ajili ya Dunia Mahiri Zaidi" kwenye Kongamano la Kimataifa la Simu Mwaka 2024 mjini Barcelona, Hispania, Februari 27, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha