

Lugha Nyingine
Tanzania na Rwanda kuboresha ushirikiano kwenye Bandari ya Dar es Salaam
(CRI Online) Machi 14, 2024
Tanzania na Rwanda zimekubaliana kuweka mazingira bora yatakayosaidia kuongeza ufanisi wa matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya njia za kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali, nchini Rwanda akiambatana na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Dkt. Vincent Biruta.
Mbali na usafirishaji, Waziri Makamba na Waziri Biruta wamejadili masuala mengine ya kipaumbele kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwemo nishati, kilimo na teknolojia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma