Baraza la Usalama lapitisha azimio la nyongeza ya kiufundi ya muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 15, 2024

Wajumbe wakipigia kura rasimu ya azimio katika mkutano wa Baraza la Usalama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Machi 14, 2024. (Eskinder Debebe/Picha ya UN/Kupitia Xinhua)

Wajumbe wakipigia kura rasimu ya azimio katika mkutano wa Baraza la Usalama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Machi 14, 2024. (Eskinder Debebe/Picha ya UN/Kupitia Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuidhinisha "nyongeza ya kiufundi" ya muda wa mamlaka ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) siku ya Alhamisi.

Azimio hilo la namba 2726, ambalo limeungwa mkono kwa kauli moja na nchi wajumbe 15 wa baraza hilo, linaamua kuongeza muda wa UNMISS hadi Aprili 30, 2024, na kuidhinisha UNMISS kutumia njia zote zinazohitajika kutekeleza majukumu yake.

Nyongeza hiyo ya kiufundi ya muda itatoa muda zaidi kwa wajumbe wa baraza hilo kutathmini maandalizi ya uchaguzi wa Sudan Kusini na kujadili kuongezwa kwa muda wa ujumbe huo, ambayo ni pamoja na kutoa msaada wa kiufundi kwa uchaguzi wa Sudan Kusini.

UNMISS kwa sasa imepewa kazi ya kutoa msaada wa kiufundi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwezo, na utoaji wa huduma kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi, pamoja na msaada wa usalama ili kuwezesha mchakato mzima wa uchaguzi.

Ripoti mpya ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan Kusini, hata hivyo, imejizuia kufanya uamuzi kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa nchi hiyo ambao uliopangwa kufanyika Desemba 2024. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha