Pendekezo la China la Ukanda Mmoja, Njia Moja lajenga njia ya ustawi wa pamoja kanda ya Afrika ya Kati

(CRI Online) Machi 18, 2024

Picha iliyopigwa Machi 15, 2022 ikionesha muonekano wa bandari ya Kribi huko Kribi, Cameroon. (Picha na Kepseu/Xinhua)

Picha iliyopigwa Machi 15, 2022 ikionesha muonekano wa bandari ya Kina Kirefu ya Kribi huko Kribi, Cameroon. (Picha na Kepseu/Xinhua)

Viongozi wa nchi za Afrika ya Kati wamekutana Jumamosi iliyopita mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, kusherehekea maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kiuchumi na Kifedha ya Nchi za Afrika ya Kati (CEMAC).

Mkutano huo umelenga kutathmini mafanikio yaliyopatikana na kupanga mikakati ya kuboresha muunganisho wa kikanda, huku msisitizo ukiwa katika kukabiliana na changamoto na fursa za ukuaji wa kiuchumi.

Kutokana na uwekezaji mkubwa na utaalamu kutoka China, nchi wanachama wa Jumuiya hiyo zimeshuhudia ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu katika sekta ya uchukuzi, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Kina Kirefu ya Kribi katika mji wa Kribi, kusini mwa Cameroon, ambayo imejengwa na kampuni ya Uhandisi wa Bandari ya China (CHEC).

Meneja mkuu wa kampuni ya CHEC kanda ya Afrika ya Kati, Xu Huajiang amesema, utandawazi na muunganisho wa kikanda vimekuwa ni mwelekeo wa kawaida wa maendeleo, na vinapaswa kukumbatiwa na nchi za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha