China na New Zealand zakubaliana kuimarisha ushirikiano na uhusiano katika muongo ujao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Winston Peters huko Wellington, New Zealand, Machi 18, 2024. (Xinhua/Guo Lei)

WELLINGTON - China na New Zealand zitafanya juhudi za pamoja za kujenga ushirikiano na uhusiano wa karibu zaidi katika muongo mmoja ujao, hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini New Zealand na mwenzake wa New Zealand Winston Peters wakati wa mazungumzo yao siku ya Jumatatu.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa sasa yuko ziarani nchini New Zealand na Australia kuanzia Machi 17 hadi 21.

Katika mkutano wake na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand Winston Peters, Wang amesema kwamba mwelekeo wa maendeleo mazuri ya uhusiano wa pande mbili licha ya mabadiliko ya hali ya kimataifa na ya kikanda imekuwa sababu ya kuleta utulivu duniani, akisisitiza kuheshimiana, kuvumiliana, kujikita katika ushirikiano na kunufaisha watu ni vichocheo vizuri vinavyostahili kufanya kazi zaidi.

Wakati mwaka huu unatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili, Wang amesema kuwa China ingependa kushirikiana na New Zealand ili kufanya mambo mengi zaidi ya kwanza katika uhusiano wa pande mbili ili uhusiano huo kutangulia katika uhusiano kati ya China na nchi zilizoendelea na kushuhudia muongo mpya wenye maendeleo makubwa zaidi.

Wang amesema, China na New Zealand zina makubaliano mengi muhimu na maslahi mapana ya pamoja, na kwamba ushirikiano wa kunufaishana siku zote nijambo kuu katika uhusiano wa pande mbili, akitoa wito kwa pande zote mbili kuendelea kuheshimu mfumo wa kijamii na njia ya maendeleo zilizochaguliwa na kila upande, na kubeba maslahi ya msingi na mambo makuu yanayofuatiliwa na kila upande.

Wang pia ametoa ufafanuzi kuhusu msimamo wa China kuhusu suala la Taiwan, na masuala yanayohusiana na Hong Kong, Xizang, Bahari ya Kusini ya China na haki za binadamu.

Kwa upande wake, Peters amebainisha kuwa China ni mwenzi muhimu wa New Zealand, na kuongeza kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili umepata maendeleo makubwa tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili miaka 10 iliyopita.

Amesema, New Zealand inafuata kwa uthabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na inatarajia kuongezeka kwa mawasiliano ya ngazi ya juu, kupanua ushirikiano katika uchumi na biashara, elimu, utamaduni na hatua za mabadiliko ya tabianchi, na kuimarisha mawasiliano na uratibu katika masuala ya kikanda na kimataifa, kusukuma mbele ukuaji wa uhusiano wa pande mbili katika muongo mmoja ujao au hata miaka 50.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Winston Peters huko Wellington, New Zealand, Machi 18, 2024. (Xinhua/Guo Lei)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Winston Peters huko Wellington, New Zealand, Machi 18, 2024. (Xinhua/Guo Lei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha