Sera ya kusameheana visa yachochea wimbi la utalii kati ya China na Thailand

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2024

Watalii wa China wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Ancient Siam huko Samut Prakan, Thailand, Machi 1, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

Watalii wa China wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Ancient Siam huko Samut Prakan, Thailand, Machi 1, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

TAIYUAN - Mara tu baada ya kuaga kundi la walimu wa Thailand waliokuwa wakitembelea vyuo vikuu mjini Beijing, muongoza watalii wa China, Yang Yaoyu alikuwa katika pilika za haraka kuelekea hadi Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China ili kukutana na kuongoza kundi lingine la wageni wa Thailand.

Mwongozo watalii huyo wa msimu anayezungumza Lugha ya Kithai anaweza kuthibitisha kuongezeka kwa shauku kwa watalii wa Thailand kutembelea China, baada ya makubaliano ya kusameheana visa kati ya nchi hizo mbili kuanza kutekelezwa Machi 1 mwaka huu.

"Hapo awali, kipindi cha watalii wa Thailand kuja kwa wingi nchini China kilikuwa mwezi Aprili baada ya Sikukuu ya Songkran. Hata hivyo, ratiba yangu sasa imejaa oda kikamilifu kuanzia Machi 3 hadi mwisho wa Aprili," Yang amesema.

Porntip Rojansunan, pamoja na wageni wengine 20 wa Thailand katika kundi lake, ni wanufaika wa msamaha wa visa. Baada ya kupanda ndege kuruka moja kwa moja kutoka Bangkok hadi Taiyuan, mji mkuu wa Shanxi, Machi 9, kundi hilo lilianza safari yao ya utalii wa siku tano kwa kutembelea maeneo matatu ya Urithi wa Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) katika mkoa huo, ambayo ni, Mlima Wutai, Mapango ya Yungang, na mji wa kale wa Pingyao.

"Hapo awali, nilikuwa nafahamu tu maeneo ya kutalii nchini China kama vile Beijing na Shanghai. Tangu nije Shanxi, sina budi kusema jinsi nilivyovutiwa na historia ya kina na utamaduni tajiri wa hapa. Bila shaka nitahimiza marafiki na jamaa zangu kuja kujionea wenyewe haiba hiyo ya Shanxi," Porntip amesema.

Sera ya kusameheana visa kati ya wasafiri wa pande mbili imeongeza mabadilishano ya kitamaduni kati ya watu wa China na Thailand, na watalii wengi zaidi wa Thailand wanaifikiria China kama kivutio chao cha kwanza cha kusafiri nje ya nchi.

Takwimu kutoka jukwaa kubwa la mtandaoni la utalii la China la Trip.com zinaonyesha kuwa Machi 1, 2024, idadi ya watalii wa China kwenda Thailand iliongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 kuliko mwaka 2023, huku oda za kusafiri kutoka Thailand hadi China zikiongezeka mara tatu kuliko mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la mara tatu kuliko mwaka 2023, na ni ongezeko la zaidi ya asilimia 160 ikilinganishwa na Mwaka 2019.

China na Thailand ni nchi muhimu zenye vivutio vya utalii na vyanzo vya watalii kwa kila upande, na utekelezaji wa msamaha wa visa kwa pande zote umechochea ushawishi mkubwa kwa ukuaji wa shughuli za utalii katika nchi zote mbili, amesema Qin Jing, naibu mkuu wa Kundi la Kampuni za Trip.com.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha