Mafunzo ya ufundi stadi na mafunzo kwa watu wenye ujuzi ni maeneo muhimu ya ushirikiano kati ya China na Angola

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2024

Picha hii iliyopigwa Mei 20, 2023 ikionyesha hafla ya kuchepusha kwa muda mkondo wa Mto Cuanza kwenye eneo la Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Caculo-Cabaca kilichojengwa na China katika Jimbo la Cuanza Norte, Angola. (Kampuni ya Gezhouba ya China/ Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 20, 2023 ikionyesha hafla ya kuchepusha kwa muda mkondo wa Mto Cuanza kwenye eneo la Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Caculo-Cabaca kilichojengwa na China katika Jimbo la Cuanza Norte, Angola. (Kampuni ya Gezhouba ya China/ Xinhua)

LUANDA - Siku ya Ijumaa mjini Beijing, Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Angola Joao Lourenco walitangaza kuinua uhusiano wa pande mbili hadi kuwa ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote.

Angola, nchi iliyoko Kusini Magharibi mwa Afrika ambayo inazungumza Lugha ya Kireno, iliyotoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 27 mwaka 2002, imeendeleza ushirikiano mzuri na China katika miongo miwili iliyopita. Sifa ya ushirikiano huu ni kufanyika katika nyanja mbalimbali, na Angola imepata maendeleo makubwa katika kujenga upya nchi, kuboresha viwanda na kuwaandaa watu wenye ujuzi.

Rais Xi alisema kwenye mazungumzo na Rais Lourenco, kuwa ushirikiano kati ya China na Angola ni ushirikiano wa Kusini na Kusini na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea. Unaelezewa kuwa wa kusaidiana kati ya marafiki wazuri, kutendeana kwa usawa na ushirikiano wa kunufaishana.

Luis Erivaldo, kijana wa Angola anayefanya kazi katika Kampuni ya Huawei, alikuwa anapenda sana teknolojia ya mawasiliano wakati akisoma shuleni. Baada ya duru nne za usaili, alijiunga na Kampuni ya Huawei, Tawi la Angola na amekua kutoka mfanyakazi mchanga hadi mkurugenzi wa kiufundi katika kipindi cha miaka sita.

Mwaka 2022, serikali ya Angola ilitia saini mkataba wa makubaliano na Huawei kwa ajili ya programu ya mafunzo ya "vipaji vya kidijitali", ambayo inapanga kutoa mafunzo kwa vijana zaidi ya 10,000 wa Angola katika miaka mitano ijayo.

Kuna wigo mpana wa ushirikiano katika elimu ya ufundi stadi kati ya China na Afrika.

Agosti 2023, Rais Xi aliongoza pamoja na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Mazungumzo ya Viongozi wa China na Afrika mjini Johannesburg, akipendekeza mipango ya kuimarisha ushirikiano wenye matokeo halisi kati ya China na Afrika na kuunga mkono mafungamanoya Afrika na kuifanya Afrika iwe ya kisasa, ukiwemo Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika juu ya mafunzo kwa watu wenye ujuzi.

Hafla ya uzinduzi wa Kituo Jumuishi cha Mafunzo ya Kiteknolojia kwa msaada wa China, ilifanyika katika Mji wa Huambo, Angola, Januari 12. Kituo hicho chenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 20,000 kina maabara 30 na karakana sita zinazohusu roboti, michakato ya mitambo, sayansi ya kompyuta na kukarabati magari. Katika awamu yake ya kwanza, kinapanga kutoa mafunzo kwa watu 2,400 kila mwaka.

Mgeni akipiga picha za simu ya mkononi iliyoonyeshwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Eneo Maalum la Teknolojia la Huawei nchini Angola, mjini Luanda, Angola, Novemba 14, 2022. (Xinhua/Lyu Chengcheng)

Mgeni akipiga picha za simu ya mkononi iliyoonyeshwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Eneo Maalum la Teknolojia la Huawei nchini Angola, mjini Luanda, Angola, Novemba 14, 2022. (Xinhua/Lyu Chengcheng)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha