WMO yatoa tahadhari nyekundu juu ya viwango vinavyovunja rekodi vya mabadiliko ya Tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2024

Watoto wakicheza kwenye chemchemi ya maji ya kujengwa na binadamu ili kupoza miili yao katika eneo la hoteli ya Sheraton huko Doha, Qatar, tarehe 6 Julai 2023. (Picha na Nikku/Xinhua)

Watoto wakicheza kwenye chemchemi ya maji ya kujengwa na binadamu ili kupoza miili yao katika eneo la hoteli ya Sheraton huko Doha, Qatar, tarehe 6 Julai 2023. (Picha na Nikku/Xinhua)

GENEVA - Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Celeste Saulo ametoa tahadhari nyekundu siku ya Jumanne wakati ambapo takwimu mpya zikionyesha kuwa viwango mbalimbali vya mabadiliko ya tabianchi vilivunja rekodi ya Mwaka 2023.

Shirika hilo, limetoa ripoti mpya kuhusu hali ya mabadiliko ya tabianchi duniani Mwaka 2023. Inaonyesha kuwa mwaka jana, rekodi zilivunjwa za viwango mbalimbali vya mabadiliko ya tabianchi kama vile viwango vya gesi joto, joto la juu ya ardhi, joto la baharini na asidi, kuongezeka kwa viwango vya bahari, kupungua kwa kifuniko cha barafu na theluji ya Bahari ya Antaktiki.

"Ripoti hii ya kila mwaka inaonyesha kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi ndiyo changamoto inayokabili binadamu," Saulo amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva. "Ina uhusiano wa karibu na janga la kukosekana kwa hali ya usawa, kama inavyoshuhudiwa na kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa usalama wa chakula, kuhama kwa watu na ukosefu wa bioanuwai."

Mawimbi ya joto, mafuriko, ukame, moto wa nyika na vimbunga vinavyoongezeka kwa kasi vya kitropiki vimesababisha taabu na gharika mwaka jana, ripoti hiyo imesisitiza, huku vikichukua maisha ya mamilioni ya watu na kusababisha hasara yenye thamani ya mabilioni ya dola katika uchumi.

WMO imethibitisha kuwa Mwaka 2023 ulikuwa mwaka uliorekodi joto la juu zaidi katika historia, ukiwa na wastani wa joto duniani wa nyuzi 1.45, na kiasi cha kutokuwa na uhakika cha nyuzi 0.12, juu ya kiwango cha zama za kabla ya maendeleo ya viwanda.

Wakati huo huo, viwango vilivyorekodiwa vya mkusanyiko wa gesi joto kuu tatu -- kaboni dioksidi, methane, na oksidi ya nitrojeni - vilifikia viwango vya kuvunja rekodi Mwaka 2022 na kuendelea kuongezeka Mwaka 2023. Viwango vya kaboni dioksidi (CO2) ni asilimia 50 zaidi kuliko zama za kabla ya maendeleo ya viwanda.

"Uwepo wa muda mrefu wa CO2 inamaanisha kuwa halijoto itaendelea kupanda kwa miaka mingi ijayo," ripoti hiyo imeonya.

Mtu akiwa amesimama pembeni mwa nyumba yake iliyofurika maji baada ya mvua kubwa kunyesha katika Kaunti ya Garissa, Kenya, Novemba 22, 2023. (Picha na Joy Nabukewa/Xinhua)

Mtu akiwa amesimama pembeni mwa nyumba yake iliyofurika maji baada ya mvua kubwa kunyesha katika Kaunti ya Garissa, Kenya, Novemba 22, 2023. (Picha na Joy Nabukewa/Xinhua)

Wazima moto wakipambana na moto katika eneo la msitu wa Serra do Coco huko Riachao das Neves, Jimbo la Bahia, Brazili, Septemba 22, 2023. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua)

Wazima moto wakipambana na moto katika eneo la msitu wa Serra do Coco huko Riachao das Neves, Jimbo la Bahia, Brazili, Septemba 22, 2023. (Picha na Lucio Tavora/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha