Mapato yanayotokana na mauzo ya nje ya Uganda yapungua kwa asilimia 8.3 katika mwezi Januari

(CRI Online) Machi 20, 2024

Wizara ya Mipango ya Kifedha na Maendeleo ya Kiuchumi ya Uganda imesema kwenye ripoti yake ya kila mwezi iliyotolewa Machi 18, kuwa katika mwezi Januari 2024, Uganda ilisafirisha nje ya nchi bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 565.40, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 8.3 ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 616.36 za mwezi uliopita.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, Wizara hiyo imesema ikilinganishwa na mwezi huo huo mwaka jana, mauzo ya bidhaa nje ya nchi yameiongezeka kwa asilimia 34.1 kutoka dola za kimarekani milioni 421.55 za mwezi Januari 2023. Hii imechangiwa na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na mauzo ya dhahabu, kahawa na uuzaji tena nje wa mafuta.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha