Eneo Maalum la Viwanda lililojengwa na China nchini Ethiopia laingiza dola za Marekani milioni 20 ndani ya miezi sita

(CRI Online) Machi 20, 2024

Serikali ya Ethiopia imeingiza dola za Marekani milioni 20 kutokana na mauzo ya bidhaa ndani ya miezi sita kupitia bidhaa zilizozalishwa katika Eneo Maalum la Viwanda la Hawassa lililojengwa na China.

Shirika la Habari la Ethiopia limemnukuu meneja mkuu wa eneo hilo, Mathiwos Ashenafi akisema, eneo hilo linatarajia kuingiza dola za Marekani milioni 44 kutokana na mauzo ya bidhaa zinazozalishwa na wazalishaji walio ndani ya eneo hilo katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, ulioanza mwezi Julai mwaka jana.

Eneo hilo lililopo kusini mwa mji wa Hawassa, kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, linachukuliwa kuwa kituo kinachoongoza kwa wazalishaji wa kigeni nchini humo, na linajihusisha na bidhaa za vitambaa na nguo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha