Australia yapenda kushirikiana na China kutafuta maslahi ya pamoja kadri iwezekanavyo: Waziri Mkuu wa Australia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2024

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese akikutana na Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye yuko ziarani nchini humo huko Canberra, Australia, Machi 20, 2024. (Picha na Chu Chen/Xinhua)

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese akikutana na Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye yuko ziarani nchini humo huko Canberra, Australia, Machi 20, 2024. (Picha na Chu Chen/Xinhua)

CANBERRA - Tofauti na kutokubaliana havipaswi kuelezea uhusiano kati ya Australia na China, na nchi hizo mbili zinapaswa kutafuta maslahi ya pamoja kadri iwezekanavyo, Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema Jumatano.

Albanese ametoa kauli hiyo alipokutana na Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye yuko ziarani nchini humo. Kuanzia Machi 17 hadi 21 Wang Yi anafanya ziara rasmi nchini New Zealand na Australia.

Australia imefurahishwa kuona kwamba katika miaka miwili iliyopita, uhusiano kati ya Australia na China umerejea kwenye mwelekeo sahihi, na Australia ingependa kuweka karibu mawasiliano ya ngazi ya juu na China na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali, amesema Albanese.

Albanese amesisitiza kuwa Australia daima inashikilia na itafuata sera ya kuwepo kwa China Moja.

Huku akibainisha vikwazo vilivyoathiri uhusiano kati ya China na Australia vimetatuliwa moja baada ya kingine, na mambo yaliyobaki yanatatuliwa, Wang amesema uhusiano kati ya China na Australia umepata mageuzi ya pili muhimu baada ya serikali ya sasa ya Australia inayongozwa na Chama cha Labor kuingia madarakani.

Wang amesema China inapenda kushirikiana na Australia kuhimiza mawasiliano ya ngazi ya juu, kurejesha upya utaratibu wa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili, na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali.

Huku akitoa mwito wa juhudi za kudhibiti na kuvuka tofauti kwa moyo wa kuheshimiana, Wang amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuhimiza kwa pamoja ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa China na Australia kuendelezwa kwa kupevuka zaidi, wenye utulivu zaidi na matunda zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha