

Lugha Nyingine
Wataalamu wa Afrika wakutana nchini Kenya kujadili njia za kuendeleza mageuzi ya kijani
Wataalamu zaidi ya 60 wa mabadiliko ya tabianchi barani Afrika wameanza mkutano wa siku tatu mjini Nairobi, Kenya, kujadili njia za kushawishi sera za mageuzi ya kijani zinazoendana na bara hilo.
Kwenye mkutano huo ulioandaliwa na jopo la washauri bingwa la Kundi la Wataalamu wa Majadiliano la Afrika, wataalamu hao wanatafuta mwelekeo utakaohakikisha kuwa rasilimali za bara hilo zinachukua nafasi yake na kutumika kikamilifu katika ajenda ya tabianchi duniani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu nchini Kenya, Festus Ngeno amesema, wataalamu hao wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja, na kuungana mkono katika masuala ya kimsingi ili kuwa na mshikamano na kutafuta matokeo mazuri kwa ajili ya Bara la Afrika.
Amesema mabadiliko ya tabianchi yameendelea kuwa tishio kubwa kwa nchi za Afrika, yakiathiri watu, maisha yao, mfumo wa ikolojia na bioanwai.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma