Ukuaji wa Pato la Taifa la Ghana wapungua Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 22, 2024

Wachuuzi wakiuza bidhaa barabarani mjini Accra, Ghana, Machi 20, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Wachuuzi wakiuza bidhaa barabarani mjini Accra, Ghana, Machi 20, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Samuel Kobina Annim, mtakwimu wa serikali wa Shirika la Takwimu la Ghana, amesema kasi ya ukuaji wa pato la taifa la Ghana (GDP) ilipungua hadi asilimia 2.9 Mwaka 2023 ambapo licha ya kasi kubwa ya ukuaji wa asilimia 3.8 katika robo ya nne ya mwaka jana, kwa ujumla kasi ya ukuaji kwa mwaka mzima ilipungua kwa asilimia 0.9 ikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa Mwaka 2022.

"Kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa kwa sekta ya viwanda kilirejea kwenye mdororo, kikikua kwa asilimia 1.2 Mwaka 2023," Annim amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Accra, mji mkuu wa Ghana siku ya Jumatano, huku akiongeza kuwa sekta ya huduma ilirekodi kiwango cha ukuaji cha asilimia 5.5 ikichangiwa zaidi na teknolojia ya habari na mawasiliano na shughuli za afya na kijamii.

“Sekta ya kilimo ilirekodi ukuaji wa mwaka hadi mwaka wa asilimia 4.5, huku mifugo na uzalishaji wa mazao vikirekodi viwango vya juu vya ukuaji kuliko wastani wa kitaifa,” ameongeza.

Ghana imekuwa ikitekeleza mageuzi ya uchumi tangu Mei mwaka jana, yakiungwa mkono na mkopo wenye thamani ya dola bilioni 3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa ili kukabiliana na changamoto nyingi za kiuchumi za muda mrefu ikiwa ni pamoja na kushuka kwa thamani ya sarafu na gharama kubwa za maisha.

Wachuuzi wakiuza bidhaa barabarani mjini Accra, Ghana, Machi 20, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Wachuuzi wakiuza bidhaa barabarani mjini Accra, Ghana, Machi 20, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha