Baraza la Boao la Asia latangaza ajenda ya mkutano wa mwaka 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 25, 2024

Picha hii iliyopigwa tarehe 22, Machi ikionesha alama ya Baraza la Boao la Asia kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa cha baraza hilo huko Boao, Mkoa wa Hainan wa China. (Xinhua/Yang Guanyu)

Picha hii iliyopigwa tarehe 22, Machi ikionesha alama ya Baraza la Boao la Asia kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa cha baraza hilo huko Boao, Mkoa wa Hainan wa China. (Xinhua/Yang Guanyu)

Mkutano wa Baraza la Boao la Asia 2024 utafanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mwezi Machi huko Boao, Mkoa wa Hainan wa China.

Mkutano huo utahusisha mkutano na waandishi wa habari unaopangwa kufanyika tarehe 26, makongamano mbalimbali na shughuli nyingine zitakazoshirikiwa na waalikwa tu, zikiwemo mikutano ya meza ya duara na mazungumzano kati ya maofisa watendaji wakuu n.k. Kutokana na ajenda iliyotangazwa kwenye tovuti ya baraza hilo, ufunguzi wa mkutano wa washiriki wote utafanyika tarehe 28, Machi.

Mwaka huu mikutano ya meza ya duara inahusu mada nyingi mbalimbali zikiwemo mada zinazofuatilia zaidi mambo ya Asia, kama vile uwekezaji wa Asia, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa Asia katika mambo ya fedha, kufanya juhudi kulijenga Asia liwe kituo cha ongezeko, n.k.

Ajenda ya mkutano imepanga majadiliano kuhusu Akili Bandia (AI), mustakabali wa magari yanayotumia nishati mpya (NEVs), ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kwenye kiwango cha juu n.k. Inatazamiwa kuwa washiriki watajadiliana lini na wapi maendeleo makubwa ya mapinduzi ya teknolojia yatatokea, mabadiliko yanayoletwa na AIGC kwa uchumi na mtindo wa maisha ya binadamu, hatari yake na usimamizi wa AI duniani kote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha