Kongamano la Wakenya waliosoma China kuhusu Pendekezo la "Ukanda Moja, Njia Moja" lafanyika Nairobi

(CRI Online) Machi 25, 2024

Kongamano la Wakenya waliosoma China kuhusu Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja ”(BRI) limefanyika mjini Nairobi, Kenya, likiwakutanisha maofisa waandamizi, wasomi na wanafunzi, ambao wamejadili athari chanya za pendekezo hilo kiuchumi na kijamii.

Kongamano hilo lililofanyika kwenye makao makuu ya kampuni ya Moja Expressway, liliandaliwa na Taasisi ya Ukanda Mmoja na Njia Moja ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing, chini ya uungaji mkono wa Kampuni ya Ujenzi wa Barabara na Madaraja ya China, CRBC.

Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Ufunguaji Mlango wa Kikanda katika Kamisheni ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China, Xu Jianping, amesema miradi ya BRI inayohusisha sekta za miundombinu, kilimo, afya na ujenzi wa uwezo imeleta manufaa kwa Kenya na bara la Afrika kwa ujumla, mbali na kuimarisha uhusiano na China. Amesema ushirikiano kati ya China na Kenya umetoa mchango muhimu katika kuongeza mawasiliano kati ya watu, kuhimiza ukuaji wa makampuni na kuchangia maendeleo ya uchumi wa China na nchi za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha