Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Nauru David Adeang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2024

Rais Xi Jinping wa China alifanya hafla ya kumkaribisha Rais David Adeang wa Nauru katika ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao hapa Beijing, China Machi 25, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

Mchana wa tarehe 25, Machi, Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo na Rais David Adeang wa Nauru ambaye yuko ziara ya kiserikali nchini China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Xi Jinping alisema, mwezi Januari mwaka huu Nauru iliamua kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na kurudisha uhusiano wa kidiplomasia kati yake na China, hali ambayo inaendana na wimbi mkubwa wa historia na nyakati. Uhusiano wa China na Nauru umefungua ukurasa mpya wa historia. China ingependa kushirikiana na Nauru katika kuanzisha mustakabali mzuri wa pamoja wa uhusiano wa nchi mbili, na kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

Xi Jinping alisisitiza kuwa, kutendeana kwa usawa ni sifa wazi ya China katika kushughulikia mambo ya nje. China siku zote ni moja kati ya nchi zinazoendelea, na kura ya China katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku zote ni ya nchi zinazoendelea. China na Nauru zina uhusiano wa kuheshimiana, kunufaishana na kuungana mkono. China inaiunga mkono Nauru bila ya kulegalega katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo, na pia inaunga mkono Nauru kufuata njia ya maendeleo kwa kujitawala na kujiamulia, njia ambayo inaendana na hali ya nchi yake. Upande wa China ungependa kuimarisha mawasiliano na upande wa Nauru katika ngazi mbalimbali na sekta mbalimbali, kuongeza maelewano na hali ya kuaminiana siku hadi siku, na kuimarisha msingi wa kisiasa wa uhusiano wa nchi mbili.

Xi Jinping alisema, China inakaribisha Nauru kutia saini kwenye nyaraka za ushirikiano na China za ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na ingependa kufanya ushirikiano wa kufuata hali halisi na Nauru katika kupanua biashara na uwekezaji, ujenzi wa miundombinu na sekta nyingine, na kutoa msaada bila ya sharti lolote la kisiasa kwa ajili ya Nauru kufikia maendeleo endelevu kwa kujitegemea.

Adeang alisema, anaona fahari kubwa kufanya ziara ya kiserikali nchini China kutoka na mwaliko. Mwaka huu Nauru ilirudisha uhusiano wa kidiplomasia na China kwenye msingi wa kutambua na kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, hali ambayo ni tukio muhimu katika uhusiano kati ya China na Nauru, nalo limefungua ukurasa mpya wa maendeleo ya Nauru na uhusiano wa nchi mbili. Nauru inasifu sana China kushikilia kutendeana kwa usawa kwa nchi zote kubwa au ndogo, na ingependa kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuendeleza kwa kina ushirikiano na China siku hadi siku.

Mchana wa tarehe 25, Machi, Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo na Rais David Adeang wa Nauru  ambaye yuko kwenye ziara ya kiserikali nchini China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. (Xinhua/Zhai Jianglan)

Marais wa China na Nauru baada ya mazungumzo yao wakishuhudia utiaji saini  wa nyaraka za ushirikiano katika kujenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, maendeleo ya uchumi, maendeleo ya kilimo n.k. (Xinhua/Liu Bin)

Rais Xi Jinping wa China alifanya hafla ya kumkaribisha Rais David Adeang wa Nauru katika ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao hapa Beijing, China Machi 25, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China alifanya hafla ya kumkaribisha Rais David Adeang wa Nauru katika ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao hapa Beijing, China Machi 25, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Rais Xi Jinping wa China alifanya hafla ya kumkaribisha Rais David Adeang wa Nauru katika ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao hapa Beijing, China Machi 25, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China alifanya hafla ya kumkaribisha Rais David Adeang wa Nauru katika ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao hapa Beijing, China Machi 25, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China alifanya hafla ya kumkaribisha Rais David Adeang wa Nauru katika ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao hapa Beijing, China Machi 25, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China alifanya hafla ya kumkaribisha Rais David Adeang wa Nauru katika ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao hapa Beijing, China Machi 25, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha