Wanaharakati wa Afrika wanasema mustakabali unaostahimili mabadiliko ya tabia nchi uko hatarini

(CRI Online) Machi 26, 2024

Wanaharakati wa Afrika wamesema mpito kwa mustakabali wa kijani, ulio wa haki na stahimilivu barani Afrika, uko hatarini kutokana na nchi zilizoendelea kupuuza ahadi za kifedha za kulisaidia bara la Afrika kukabiliana na msukosuko wa mabadiliko ya tabia nchi.

Wanaharakati hao waliokutana jana kwenye kongamano mjini Nairobi, wamesema licha ya bara la Afrika kuchangia chini ya asilimia 4 ya utoaji wa hewa chafu duniani, bara hilo linabeba mzigo mkubwa wa kuongezeka kwa hali joto duniani na uwezo mdogo wa kifedha na kiufundi wa kukabiliana na hali hiyo.

Mratibu mkuu wa Shirika la usalama wa Chakula barani Afrika (AFSA), Million Belay, amesema bara la Afrika linapaswa kudai sehemu ya haki ya fedha za kimataifa zinazolenga kukabiliana na mabadiliko hayo.

Naibu mkurugenzi katika Wizara ya Mazingira ya Kenya, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu Bw. Michael Okumu, amesema nchi za Afrika zinafuatilia kwa makini utekelezaji wa maazimio muhimu ya mkutano wa COP28, ikiwa ni pamoja na utoaji wa fidia kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, ambazo ni muhimu katika kuandaa mpito wa kijani katika bara la Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha