Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya ndani na nje ya China wajisajili kwa ajili ya Mkutano wa Baraza la BOAO 2024

By Aris (Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2024

C:\Users\hp\Desktop\1.jpg

Wafanyakazi wakionekana kwenye dawati la kituo cha waandishi wa habari kujisajili kwa ajili ya Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 katika Kisiwa cha Boao, Mkoa wa Hainan Kusini mwa China, Machi 25, 2024. (People's Daily Online)

Ukiwa na kaulimbiu isemayo "Asia na Dunia: Changamoto za Pamoja, Kuchangia wajibu," Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 utaanza kufanyika kuanzia Machi 26 hadi 29 katika mji mdogo wa Boao ulioko Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji, mkutano huo utahudhuriwa na wageni mbalimbali mashuhuri wakiwemo maofisa waandamizi wa sasa na wa zamani wa serikali za nchi na maeneo mbalimbali, wakuu wa mashirika ya kimataifa pamoja na viongozi wa kibiashara kutoka kampuni za ndani ya China na za kimataifa. Pia wasomi, washauri bingwa, watunga sera na wadau mbalimbali wamejiandikisha kuhudhuria na kushiriki majukwaa madogo mbalimbali.

Katika mkutano huo kutakuwa na majukwaa mbalimbali madogo ambapo mada mbalimbali kama vile kuwekeza katika siku za baadaye za Asia, kuukabili mgawanyiko katika biashara ya kimataifa, kuendeleza kasi ya kuhamia kuelekea nishati ya kaboni sifuri, mustakabali wa magari yanayotumia nishati mpya, usimamizi wa kijamii na usalama wa kikanda, kuzidisha ushirikiano wa kifedha katika Asia, kuharakisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na nyingine nyingi zitawasilishwa na kujadiliwa.

C:\Users\hp\Desktop\2.jpg

Waandishi wa habari wakijisajili kwa ajili ya kushiriki kwenye mkutano wa mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 katika Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 25, 2024. (People's Daily Online)

C:\Users\hp\Desktop\3.jpg

Waandishi wa habari wakijisajili kwa ajili ya kushiriki kwenye mkutano wa mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 katika Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 25, 2024. (People's Daily Online)

Bango la Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 likionekana nje ya kituo cha waandishi wa habari kujisajili kwa ajili ya mkutano huo katika Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 25, 2024 (People’s Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha