Idadi ya vifo katika shambulizi la kigaidi huko Moscow yaongezeka hadi 139

(CRI Online) Machi 27, 2024

Mkuu wa kamati ya upelelezi ya Russia Bw. Alexander Bastrykin amesema idadi ya vifo kutokana na shambulizi la kigaidi lililofanywa na watu wenye silaha Ijumaa iliyopita dhidi ya ukumbi wa muziki mjini Moscow imeongezeka na kufikia 139.

Upelelezi uliofanywa na kamati hiyo umefanikiwa kujua mpangilio kamili wa shambulizi hilo, na matokeo ya awali ya uchunguzi yanaonesha kuwa shambulizi hilo la kigaidi lilipangwa na kutayarishwa kikamilifu.

Mapema jumatatu kamati hiyo iliomba kukamatwa kwa washukiwa wengine watatu waliowapa magaidi hao nyumba na gari, na kusafirisha pesa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha