Rais wa zamani wa Slovenia asema kutengana kiuchumi na kuondoa hatari kunamaanisha kupoteza faida za utandawazi zilizopatikana kwa bidii

By Aris (Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2024

C:\Users\hp\Desktop\1.jpg

Danilo Türk (kwenye skrini), Rais wa zamani wa Slovenia na Rais wa sasa wa Klabu ya Madrid akizungumza kwenye jukwaa dogo la Mtazamo wa Siasa za Kijiografia Kimataifa chini ya Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 hapa Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 27, 2024. (Picha/People's Daily Online)

Danilo Türk, ambaye alikuwa rais wa zamani wa Slovenia na kwa sasa ni rais wa Klabu ya Madrid, amesema kuwa dhana za "kutengana" na "kuondoa hatari" zilizoanzishwa hivi karibuni katika uchumi na biashara ya kimataifa zinaifanya Dunia kupoteza kile kilichopatikana katika kipindi cha utandawazi mkubwa.

Türk pia ameonya kwamba, vile vinavyohimizwa sana na nchi za Magharibi vya "utaratibu unaozingatia kanuni" na "maadili ya dunia" haviko wazi, vinachangia zaidi katika mkanganyiko wa kimataifa.

Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wa People's Daily Online Jumatano, Machi 27 wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 unaoendelea hapa Boao, China, Türk amesema kuwa kutengana kiuchumi tayari kunaonyesha athari mbaya na kwamba Dunia haipaswi kupoteza kile kilichopatikana katika kipindi cha utandawazi mkubwa.

"Nadhani kutengana tayari kunaonyesha athari zenye shida, na hatupaswi kupoteza kile kilichopatikana katika kipindi cha utandawazi mkubwa" Türk amesema.

Amesema kuwa, Dunia inahitaji utaratibu ambao kutakuwa na njia ya kusaidia kila mtu kuchukua fursa na kunufaika, na aliongeza kwamba ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote ni dhana nzuri sana lakini kutengana hakutumikii dhana hiyo.

Kwa "kuondoa hatari katika uchumi na biashara", ambayo pia ni dhana inayoenezwa na nchi za magharibi ikilenga kufanya biashara na China au uhusiano mwingine wa kiuchumi na China, Türk amesisitiza kwamba, kwa asili biashara au wafanyabiashara wameunganishwa na hatari na siyo lazima kuambiwa na wanasiasa kuondoa hatari.

“Biashara, wafanyabiashara wanashughulika na hatari, saa 24 kwa siku, siku 365 kwa mwaka, hatari ni asili katika ushirikiano wa kibiashara, kwa hivyo siyo lazima kuambiwa na wanasiasa kuondoa hatari, watajua hatari ni nini na jinsi ya kushughulikia hatari” Türk amesema.

Amesema kuwa, "kuondoa hatari" kama kauli mbiu ya kisiasa haina usaidizi na haifai kutumika, badala yake biashara zinapaswa kuruhusiwa kufanya kile zinachoweza kufanya ili kupunguza hatari na kufanya kila linalowezekana, na kwamba mfumo kazi wa kisera ambao taasisi za kimataifa na serikali zinaweza kuuweka haupaswi kuhamasishwa na kuondoa hatari bali kwa kuweka nafasi kwa biashara kushirikiana kwa faida zao za pande zote.

Akijibu swali kuhusu dhana za "utaratibu unaozingatia kanuni" na "maadili ya Dunia" ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikitumiwa na nchi za magharibi, Türk amesema amekuwa akitilia shaka dhana hizi kwa muda mrefu.

"Nimekuwa nikitilia shaka msamiati wa ‘utaratibu unaozingatia kanuni’, hauko wazi vya kutosha. Kanuni zipi? Kanuni ipi? Kanuni za nani? Haiko wazi.” Türk amesema.

Amesisitiza kuwa kinachopaswa kufanywa ni kuzungumzia kanuni za sheria ya kimataifa ambazo zimeanzishwa na sheria ya kimataifa na mfumo wa taasisi za kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Biashara Duniani, na taasisi za fedha za kimataifa.

"Tuna kanuni na taasisi zote za kisheria za kimataifa, lazima tuzungumze juu yao, na 'utaratibu unaozingatia kanuni' unachangia tu kwenye mkanganyiko, na kuna mkanganyiko mkubwa siku hizi," amesema.

“Kuhusu 'maadili ya Dunia', nadhani kuna maadili ya Dunia yaliyowekwa na taasisi za kimataifa, ambayo yanakubalika na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa,” Türk amesema hayo na alitoa mfano wa kukataza aina zote za ubaguzi wa rangi chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi wa rangi.

“Kwa hiyo hapa tunayo wazi hali ya maadili ya Dunia, lakini tunaona wazi pia maadili hayo hayafuatwi na wale wanaodai kuwa watetezi wa 'maadili ya Dunia'. Tunaona kwamba ubaguzi wa rangi umekithiri katika maeneo mengi duniani, hivyo mtu anatakiwa kuwa makini anapozungumzia maadili ya Dunia” ameonya.

C:\Users\hp\Desktop\2.jpg

Danilo Türk (kwenye skrini), Rais wa zamani wa Slovenia na Rais wa sasa wa Klabu ya Madrid akizungumza kwenye jukwaa dogo la Mtazamo wa Siasa za Kijiografia Kimataifa chini ya Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 hapa Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 27, 2024. (Picha/People's Daily Online)

C:\Users\hp\Desktop\3.jpg

Danilo Türk (wa pili, kulia), Rais wa zamani wa Slovenia na Rais wa sasa wa Klabu ya Madrid akishiriki kama mwanajopo kwenye jukwaa dogo la Mtazamo wa Siasa za Kijiografia Kimataifa chini ya Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 hapa Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 27, 2024. (Picha/People's Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha