Bassirou Diomaye Faye athibitishwa kuwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa Senegal

(CRI Online) Machi 28, 2024

Mgomebea wa muungano wa upinzani wa Senegal Bw. Bassirou Diomaye Faye, ameshinda uchaguzi mkuu wa Senegal kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Kuhesabu Kura Jumatano wiki hii.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Amady Diouf amesema kwenye mkutano na wanahabari kwamba Bw. Faye amepata kura milioni 2,43 ambazo ni asilimia 54.28 ya jumla ya kura. Watu walioshiriki kwenye upigaji kura ni asilimia 61.30 ya watu waliojiandikisha kupiga kura. Mpinzani wake mkuu kutoka muungano tawala Amadou Ba amepata asilimia 35.79 ya kura zote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha