China yaibuka kuwa chanzo kikuu cha uwekezaji wa kigeni nchini Tanzania

(CRI Online) Machi 28, 2024

China imekuwa chanzo kikuu cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDl) nchini Tanzania, na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi hiyo.

Hayo yamesemwa wakati wa ufungaji wa kongamano la siku moja la Uwekezaji kati ya China na Tanzania lililofanyika mjini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya rais Mipango na Uwekezaji Bi. Tausi Kida amesema kuanzia Januari 2021 hadi Desemba 2023, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilisajili miradi 256 kutoka China yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.5.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta binafsi ya Tanzania Bibi Angelina Ngalula amesema Tanzania imeboresha mazingira ya uwekezaji na kuvutia miradi ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 11 inayoongozwa na uwekezaji wa China, na kutoa nafasi za ajira 114,726.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amepongeza azma na hatua madhubuti za serikali ya Tanzania katika kuvutia uwekezaji na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha