"Tuonane Tena Nchini China" | Kila siku ukiwa Guangxi hujionea jambo jipya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 29, 2024

Waandishi wa habari 13 wa kigeni kutoka "Ziara ya Waandishi wa Habari wa nchi mbalimbali nchini China: Kukusanya habari kuhusu ujenzi huko Guangxi wa Mambo ya Kisasa ya China” walitembelea Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China.

Catherine Gulua, mwandishi wa habari mwenye uzoefu wa miaka 20 kutoka Georgia, ambaye pia ni mwanzilishi na msimamizi mkuu wa Media Center "MTAVARI" katika nchi yake. Safari hii ni ziara yake ya pili nchini China.

Akijumuika naye ni Abubakar Harith, mwanahabari kijana na mtangazaji wa TV kutoka Tanzania. Catherine na Abubakar walikutana kwa mara ya kwanza nchini China wakati wa Mkutano wa tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja uliofanyika Beijing Oktoba 2023. Safari yao ya kuelekea Guangxi ilikuwa mara ya pili kwao kukutana. Walitembelea maeneo ya mandhari nzuri katika vijiji vya kabila la Wamiao, kutembelea viwanda vyenye teknolojia za kisasa vya utengenezaji wa magari, na kuzunguka-zunguka katika mitaa iliyosafishwa na mvua ya Guilin, wakipata kumbukumbu zisizoweza kusahauliwa nao juu ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha