China na Nchi za Asia ya Kati zaanzisha sekretarieti ya mfumo wa ushirikiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2024

Wawakilishi wa China na nchi tano za Asia ya Kati wakishiriki kwenye hafla ya  kuanzishwa kwa sekretarieti ya  mfumo wa ushirikiano kati ya China na Asia ya Kati mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Machi 30, 2024. (Xinhua/Zou Jingyi)

Wawakilishi wa China na nchi tano za Asia ya Kati wakishiriki kwenye hafla ya kuanzishwa kwa sekretarieti ya mfumo wa ushirikiano kati ya China na Asia ya Kati mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Machi 30, 2024. (Xinhua/Zou Jingyi)

XI'AN - China na nchi tano za Asia ya Kati, ambazo ni Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan, zimefanya hafla ya kuanzishwa kwa sekretarieti ya mfumo wa ushirikiano kati ya China na Asia ya Kati huko Xi'an mkoani Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China siku ya Jumamosi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kazakhstan Murat Nurtleu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kyrgyzstan Jeenbek Kulubaev, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tajikistan Sirojiddin Muhriddin, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Turkmenistan Rashid Meredov, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uzbekistan Bakhtiyor Saidov walituma barua zao za pongezi.

Wang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amepongeza ushirikiano kati ya China na nchi za Asia ya Kati chini ya mfumo wa China na Asia ya Kati ambao ulianzishwa miaka minne iliyopita.

Wang amesema kuanzishwa kwa sekretarieti hiyo kunaonesha kwamba maoni ya kauli moja yaliyofikiwa na wakuu wa nchi za China na Asia ya Kati yametekelezwa na kudhihirisha kwa jumuiya ya kimataifa dhamiri ya kithabiti ya nchi hizo sita kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maendeleo na ushirikiano.

“Inaaminika kuwa kwa uungaji mkono wa pande zote, sekretarieti hiyo itafanya kazi vizuri na kwa ufanisi, na mfumo wa ushirikiano wa China na Asia ya Kati utaimarika na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi sita,” Wang ameongeza.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tano za Asia ya Kati wamesema kuwa pande zinazohusika zina matumaini makubwa kwa sekretarieti hiyo na zitaunga mkono kikamilifu kazi yake. Wameeleza matumaini yao kwamba kuanzishwa kwa sekretarieti hiyo kutaongeza kasi mpya katika ushirikiano kati ya nchi za Asia ya Kati na China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha