Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais Mteule wa Indonesia Prabowo Subianto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 02, 2024

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais mteule wa Jamhuri ya Indonesia Prabowo Subianto kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Aprili 1, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais mteule wa Jamhuri ya Indonesia Prabowo Subianto kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Aprili 1, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais Mteule wa Jamhuri ya Indonesia na Mwenyekiti wa Chama cha Vuguvugu la Indonesia Kuu Prabowo Subianto, ambaye yuko ziarani nchini China, siku ya Jumatatu, ambapo amempongeza kwa kushinda uchaguzi wa rais nchini Indonesia na kumwomba kupeleka salamu za dhati na za kumtakia kila la kheri Rais Joko Widodo.

Huku akikumbuka uhusiano wa pande mbili unaoendelea kwa kasi na wenye matunda katika muongo mmoja uliopita chini ya uongozi wa wakuu wa nchi hizo mbili, Rais Xi amesema pande zote mbili zimeifanya Reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung kuwa kielelezo cha ushirikiano wa kiwango cha juu wa pande mbili na kuingia katika hatua mpya ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

China inautendea uhusiano wake na Indonesia kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na ingependa kuzidisha ushirikiano wa kimkakati na Indonesia kwa pande zote, Rais Xi amesema.

Amesema China itashirikiana na Indonesia kujenga jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakabali wa pamoja ambayo ina ushawishi wa kikanda na kimataifa, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili na kuchangia amani, utulivu na ustawi wa kikanda na Dunia.

Rais Xi amesema jambo la msingi la mafanikio ya uhusiano kati ya China na Indonesia ni kutilia maanani kujiamulia kimkakati, kuaminiana na kusaidiana, kufanya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote, na kuwa na haki na usawa.

Pande hizo mbili zinapaswa kufuata kwa uthabiti njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi, kuungana mkono kithabiti katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo, na kuelewana na kuungana mkono katika masuala yanayohusu masilahi ya msingi na yale yanayofuatiliwa na kila mmoja wao, Rais Xi amesema.

Prabowo amewasilisha salamu za dhati za Rais Joko Widodo kwa Rais Xi, na akisema, anafuraha kuifanya China kuwa nchi ya kwanza anayoitembelea baada ya kuchaguliwa kuwa rais.

China ni nchi yenye ushawishi mkubwa, na nchi hizo mbili daima zinaheshimiana na kutendeana kwa sawa, ameongeza.

Ameeleza kufurahishwa na mafanikio makubwa waliyopata watu wa China chini ya uongozi wa Rais Xi. Amesema angependa kujifunza kutoka kwa uzoefu wa Chama cha Kikomunisti cha China na kuzidisha mabadilishano ya uzoefu wa utawala wa nchi.

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais mteule wa Jamhuri ya Indonesia Prabowo Subianto kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Aprili 1, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais mteule wa Jamhuri ya Indonesia Prabowo Subianto kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Aprili 1, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha