Ofisa wa China Bara anayeshughulikia masuala ya Taiwan akutana na Ma Ying-jeou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 02, 2024

Song Tao, Mkuu wa Ofisi ya Kazi ya Taiwan ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni  Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, akikutana na Ma Ying-jeou, mwenyekiti wa zamani wa  Chama cha Kuomintang cha China, huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 1, 2024. (Xinhua/Chen Yehua)

SHENZHEN - Song Tao, Mkuu wa Ofisi ya Kazi ya Taiwan ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, amekutana na Ma Ying-jeou, mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Kuomintang cha China, huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. Ma, ambaye anaongoza ujumbe wa vijana kutoka eneo la Taiwan kutembelea China Bara, amewasili Shenzhen siku ya Jumatatu.

Song ametoa salamu kwa Ma kutoka kwa Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.

Song amesema watu wa pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan wote ni Wachina, na wanapaswa kutilia maanani Makubaliano ya Mwaka 1992 na kupinga kwa uthabiti shughuli za kuifanya " Taiwan ijitenge " na uingiliaji wa nje.

Ametoa wito kwa watu wa pande mbili za Mlango wa Bahari wa Taiwan kuendeleza mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, kuendeleza kwa pamoja utamaduni wa China, kuimarisha udugu na ustawi wa watu wa pande mbili za Mlango wa Bahari huo, kuhimiza maendeleo ya amani na jumuishi ya uhusiano wa kuvuka Mlango Bahari wa Taiwan na kufanya jitihada kwa ajili ya muungano wa taifa, na ustawishaji wa Taifa la China.

Ma amemshukuru katibu mkuu wa chama Xi kwa salamu zake. Huku akisema kwamba watu wa pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan wana uhusiano wa karibu wa damu, ametoa wito wa kuhimizwa kwa mawasiliano na ushirikiano wa kuvuka Mlango-Bahari, hasa miongoni mwa vijana, katika msingi wa kisiasa wa kushikilia Makubaliano ya Mwaka 1992 na kupinga kuifanya "Taiwan ijitenge."

Ma Ying-jeou, mwenyekiti wa zamani wa  Chama cha Kuomintang cha China, ambaye anaongoza ujumbe wa vijana kutoka eneo la Taiwan kutembelea China Bara, akiwasili Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 1, 2024. (Xinhua/Chen Yehua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha