China kuchukua hatua kali za kulipiza endapo Marekani itaweka vizuizi vya visa kwa maofisa kutoka Hong Kong

(CRI Online) April 02, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, China itachukua hatua kali za kulipiza kama Marekani itaweka vizuizi vya visa kwa maofisa wa Hong Kong.

Wang amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari ikiwa ni majibu ya tangazo la Marekani kuwa inachukua hatua za kuweka vizuizi vipya vya visa kwa maofisa wa Hong Kong.

Wang amesema, ripoti hiyo iliyotolewa tena na Marekani mwaka huu, imeshambulia na kuichafua Sheria ya Kulinda Usalama wa Taifa katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, na pia mfumo wa uchaguzi wa Hong Kong na Mpango wa Kulinda Usalama wa Taifa.

Wang amesema, Marekani imeshusha hadhi demokrasia, utawala wa kisheria, haki za binadamu na uhuru wa Hong Kong, na kutangaza kuweka vizuizi vipya vya visa kwa maofisa wa Hong Kong, hatua ambayo ni wazi haina msingi wowote, na hakuna madai kati ya hayo yanayojikita katika ukweli.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha