Raia watatu wa kigeni wauawa katika mashambulizi ya anga ya Israel katikati ya Ukanda wa Gaza

(CRI Online) April 02, 2024

Ofisi ya habari ya kundi la Hamas imesema, watu watano wakiwemo raia watatu wa kigeni wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Israel siku ya Jumatatu katikati ya Ukanda wa Gaza.

Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo imesema, raia hao wa kigeni waliouawa ni wafanyakazi wa shirika la kutoa misaada la "World Central Kitchen", na wanatokea Uingereza, Poland na Australia.

Watu wengine wawili waliouawa katika mashambulizi hayo ya anga ni pamoja na raia mmoja wa Palestina na utambulisho wa mwingine bado haujathibitishwa. Hadi sasa Israel bado haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na idara ya afya ya Ukanda wa Gaza wa Palestina, operesheni za kijeshi za Israel katika eneo hilo katika saa 24 zilizopita zimesababisha vifo vya watu 63 na wengine 94 kujeruhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha