Lugha Nyingine
Suminwa ateuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa DRC
(CRI Online) April 02, 2024
Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesema, Judith Tuluka Suminwa ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Suminwa ambaye alikuwa Waziri wa Mipango tangu mwezi Machi mwaka jana, ameingia katika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini DRC.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuteuliwa, Bi. Suminwa amesema kazi iliyo mbele yake ni ngumu na changamoto ni nyingi, lakini amesema kwa kuungwa mkono na rais wa nchi hiyo pamoja na umma, watafanikiwa kuzikabili.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma