Waziri Mkuu wa Pakistani atembelea kambi ya mradi wa Dasu kuwapa pole wafanyakazi wa China walioshambuliwa na magaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2024

Picha hii iliyotolewa na Idara ya Habari ya Vyombo vya Habari ya Pakistani (PID) ikimuonyesha Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif akipeana mkono na mfanyakazi wa China kwenye kambi ya mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Maji wa Dasu katika Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, Pakistan, Aprili 1, 2024. (PID/Xinhua)

Picha hii iliyotolewa na Idara ya Habari ya Vyombo vya Habari ya Pakistani (PID) ikimuonyesha Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif akipeana mkono na mfanyakazi wa China kwenye kambi ya mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Maji wa Dasu katika Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, Pakistan, Aprili 1, 2024. (PID/Xinhua)

ISLAMABAD - Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif Jumatatu alitembelea kambi ya mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Maji wa Dasu katika Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo ambapo wakati akiwahutubia wafanyakazi wa mradi huo, amewaomboleza watu waliofariki katika shambulio la kigaidi la Dasu na kuwapa pole kwa dhati jamaa za waathiriwa na wafanyakazi wa China katika mradi huo.

Ni jukumu la serikali ya Pakistan kulinda usalama wa kaka na dada zetu wa China waliokuja Pakistan kutoa msaada katika maendeleo yetu, Waziri Mkuu huyo amesema, na kuahidi kuwa serikali yake itawasaka wahalifu hao na kufanya juhudi zote kulinda usalama wa raia na miradi ya China nchini Pakistan.

"Jaribio lolote la kudhoofisha urafiki kati ya nchi zetu mbili halitafanikiwa, na adui yeyote yake atashindwa vibaya," ameongeza.

Pakistan itapambana na ugaidi na kuwaadhibu vikali magaidi ili kuhakikisha kuwa matukio kama haya hayatatokea tena, Sharif amesema.

Katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Pakistan Jiang Zaidong amesema China inatumai na kuamini kuwa Pakistan itatekeleza sera yake kwa vitendo madhubuti, kuwafikisha wauaji kwenye vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo, kuondoa kikamilifu vikosi vya kigaidi, na kufanya kila juhudi kulinda usalama wa wafanyakazi, taasisi na miradi ya China nchini Pakistan.

"Tuko tayari kuimarisha ushirikiano na Pakistan katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na ugaidi, na kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Pakistan," amesema balozi wa China.

Wachina watano na raia mmoja wa Pakistani waliuawa Machi 26 katika shambulio la kigaidi kwenye njia ya kuelekea Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Maji wa Dasu katika Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa lililoko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo kutoka Islamabad.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha