Naibu Waziri Mkuu wa China azungumzana na Waziri wa Fedha wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2024

He Lifeng, naibu waziri mkuu wa China  ambaye pia ni mkurugenzi wa upande wa China wa mambo ya uchumi na biashara ya China na Marekani akifanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen tarehe 5, Aprili, 2024 mjini Guangzhou, China. (Xinhua/Mao Siqian)

He Lifeng, naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni mkurugenzi wa upande wa China wa mambo ya uchumi na biashara ya China na Marekani akifanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen tarehe 5, Aprili, 2024 mjini Guangzhou, China. (Xinhua/Mao Siqian)

He Lifeng, naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni mkurugenzi wa upande wa China wa mambo ya uchumi na biashara ya China na Marekani, alifanya mazungumzo ya duru kadhaa na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen siku ya Ijumaa na Jumamosi katika mji wa Guangzhou wa China.

Pande mbili zilifanya majadiliano kuhusu hali ya jumla ya uchumi wa nchi hizo mbili na dunia, uhusiano wa kiuchumi kati ya China na Marekani, changamoto zinazoikabili dunia nzima na masuala mengine kwenye msingi wa kutekeleza maoni muhimu ya pamoja ya marais wa nchi hizo mbili

Pande hizo mbili zilikubaliana kujadili masuala kuhusu ongezeko la uwiano la uchumi wa Marekani na China na Dunia nzima, utulivu wa mambo ya fedha, mambo ya fedha yenye maendeleo endelevu, na ushirikiano katika kutakatisha fedha chini ya uongozi wa kikundi cha kazi ya uchumi na mambo ya fedha cha China na Marekani. Upande wa China umeeleza ufuatiliaji wake mkubwa juu ya hatua za Marekani za kuzuia China katika sekta ya uchumi na biashara, na imejibu vya kutosha suala kuhusu uwezo wa uzalishaji. Pande zote mbili zimekubaliana kuendelea kudumisha mawasiliano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha