Tanzania kuimarisha usalama mtandaoni kuelekea uchumi wa kidigitali

(CRI Online) April 07, 2024

Serikali ya Tanzania inaendelea kujiimarisha kuelekea kwenye uchumi wa kidigitali kwa kuongeza nguvu kwenye usalama wa mitandao kwa ajili ya kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji.

Hayo yamefahamika kwenye mkutano wa tatu wa Jukwaa la Usalama wa Mtandao lililokutanisha wataalamu na wadau wa mambo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), na wa kutoka Ujerumani na Uswisi kujadili changamoto na kupata uzoefu wa namna ya kuboresha usalama wa kimtandao.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Tanzania, Dk Moses Nkundwe amesema lengo la jukwaa hilo ni kuona namna Tanzania inavyoweza kuwa salama zaidi kwenye mambo ya kijamii na biashara bila kudukuliwa na wahalifu wa mtandao wa Internet.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha