Huawei yafanya kongamano la teknolojia ya simu kuonesha bidhaa na huduma nchini Zambia

(CRI Online) April 07, 2024

Kampuni kubwa ya mawasiliano ya habari ya China Huawei imefanya kongamano dogo la teknolojia ya simu kuonesha utatuzi wake wa teknolojia na huduma mbalimbali kwa wateja wake.

Kongamano hilo la siku mbili lenye kaulimbiu ya “Kuharakisha shughuli ya TEHAMA nchini Zambia” ni mwendelezo wa Maonesho ya Teknolojia ya Simu Duniani yaliyofanyika huko Barcelona, Hispania mwezi uliopita, ambayo yaliwaleta pamoja maofisa kutoka serikali, makampuni za huduma za simu za mikononi na TEHAMA.

Mkurugenzi mtendaji wa uendeshaji biashara wa Huawei kanda ya kusini mwa Afrika ya jangwa la Sahara Bw. Samuel Chen amesema, katika kongamano hilo, wametafuta fursa zitakazowezesha Zambia kufanya ushindani duniani katika zama ya kidijitali.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo inalitumia kongamano hilo kuonesha jinsi Zambia inavyoweza kuhimiza maendeleo ya biashara ndogondogo na zenye ukubwa wa kati kupitia utatuzi wa teknolojia za mambo ya fedha, kuonesha utatuzi wa data wenye uvumbuzi, pamoja na kuonesha kuwa maendeleo endelevu yanaweza kutimizwa kupitia utatuzi wa nishati ya kijani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha