Waziri Mkuu wa China akutana na Waziri wa Fedha wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 7, 2024. (Xinhua/Yan Yan)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 7, 2024. (Xinhua/Yan Yan)

BEIJING- Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen siku ya Jumapili mjini Beijing ambapo amesema kuwa ni matumaini kuwa Marekani itafuata kanuni za msingi za uchumi wa soko huria ikiwa ni pamoja na ushindani wa haki na ushirikiano wa wazi, kujiepusha kugeuza masuala ya kiuchumi na kibiashara kuwa masuala ya kisiasa au kiusalama, na kutazama bila upendeleo suala la uwezo wa uzalishaji na upembuzi katika mtazamo wa soko na wa dunia.

Maendeleo ya sekta ya nishati mpya ya China yatatoa mchango mkubwa kwa Dunia kuhamia katika maendeleo ya kijani na kutoa kaboni chache, Waziri Mkuu Li ameongeza.

Huku akisisitiza kwamba uhusiano kati ya China na Marekani unaanza kutuliza chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, Waziri Mkuu Li amesema kuwa China inatumai kuwa nchi hizo mbili zitakuwa washirika, siyo maadui, zikiheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kuwa na ushirikiano wa kunufaishana.

China inatumai Marekani itashirikiana na China kuendelea kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi mbili, na kuifanya maafikiano yaliyofikiwa mjini San Francisco iwe halisi, amesema.

Ameeleza kuwa, zikiwa nchi mbili kubwa kiuchumi duniani, China na Marekani zina maslahi ya kiuchumi yaliyofungamana kwa kina, na kuongeza kuwa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kuna umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya kila upande na ukuaji wa uchumi wa Dunia.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano ili kutafuta kwa pamoja njia za kudhibiti na kutatua tofauti, ili kuufanya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa China na Marekani uwe thabiti, mzuri na wenye ufanisi, uwe na manufaa zaidi kwa kampuni na watu wa nchi hizo mbili, na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Dunia na kuboresha maisha ya watu.

Kwa upande wake Yellen amesema kwa juhudi za pamoja za pande mbili, uhusiano kati ya Marekani na China umekuwa thabiti zaidi na kwamba zikiwa nchi mbili kubwa kiuchumi duniani, Marekani na China zinapaswa kusimamia uhusiano wao wa kiuchumi wa pande mbili kwa uwajibikaji.

Amesema Marekani inathamini maendeleo yaliyopatikana katika mazungumzo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Marekani na China, haitafuti "kutengana kiuchumi" na China, na inapenda kushirikiana na China kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili mjini San Francisco, kuwasiliana kwa uwazi, kuepuka hali ya kutoelewana, kuzidisha mawasiliano na ushirikiano, kudhibiti ipasavyo tofauti, kukabiliana kwa pamoja na changamoto kubwa za kimataifa na kukuza maendeleo thabiti ya uhusiano wa pande mbili.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 7, 2024. (Xinhua/Yan Yan)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 7, 2024. (Xinhua/Yan Yan)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha