Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi asisitiza ushirikiano kati ya China na ASEAN, China na Vietnam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2024

NANNING - Wang Yi, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesisitiza kuendelea kuimarisha ujenzi wa forodha za mpakani na kuendelea kuweka msukumo mpya katika kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa Mkoa wa Guangxi wa China na ushirikiano kati ya China na ASEAN, na kuwezesha ujenzi wa masoko ya ndani na ya kimataifa.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, ameyasema hayo siku ya Ijumaa alipofanya ziara ya kukagua Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China.

Katika ziara hiyo, Wang alitembelea miradi husika ya ushirikiano kati ya China na ASEAN na China na Vietnam.

Wang amesema, ni muhimu kuhudumia kwa juhudi kubwa ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na ASEAN, kukuza kwa pamoja ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kung'arisha chapa ya dhahabu ya Maonesho ya China na ASEAN, na kujenga njia kuu ya kimataifa iliyo wazi kwa ASEAN.

Wang amesisitiza kwamba Guangxi inapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati yake na Vietnam, kujumuisha maoni ya umma na msingi wa kijamii wa urafiki kati ya China na Vietnam, kuboresha muunganisho wa miundombinu ya kuvuka mpaka, kujitahidi kujenga forodha ya mpakani yenye kujumuisha utendaji wa busara na wenye urahisi, maendeleo mengi, mawasiliano ya kirafiki, na usalama wa pande zote, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Vietnam inayobeba umuhimu wa kimkakati.

Wang amesema kuwa juhudi zaidi zitafanywa kuusaidia Mkoa wa Guangxi kuhimiza muunganisho wa nje, kutoa mafunzo kwa watu zaidi wanaoshughulikia mambo ya nje, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa, na kuusaidia mkoa huo kuharakisha maendeleo yenye sifa bora.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha