Idadi ya Magari yanayopita Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao yavunja rekodi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2024

Picha hii iliyopigwa tarehe 6 Aprili 2024 ikionyesha magari kwenye Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao, Kusini mwa China. (Picha na Wang Xiangguo/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa tarehe 6 Aprili 2024 ikionyesha magari kwenye Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao, Kusini mwa China. (Picha na Wang Xiangguo/Xinhua)

GUANGZHOU – Katika Bandari ya Zhuhai ya Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao, Kusini mwa China, kuna magari 19,570 yaliyopita katika daraja hilo siku ya Jumamosi, likifikia rekodi mpya ya juu ya idadi kubwa ya magari yanayopita kila siku kwa mara ya tatu katika muda wa siku saba, takwimu rasmi zimeonyesha.

Kuanzia Machi 28 hadi Aprili 6, kuna abiria zaidi ya milioni 1 na magari 170,000 kuingia na kutoka kwenye bandari hiyo, kama ilivyoripotiwa na forodha ya Zhuhai ya daraja hilo, ambalo ni kivuko kirefu zaidi duniani cha kuvuka bahari kwa daraja-na-handaki.

Forodha hiyo imesema, katika kipindi hicho, idadi ya jumla ya watalii wa Hong Kong na Macao ilizidi 740,000, na magari ya Hong Kong na Macao yalifikia karibu 110,000.

Watu wa Familia moja moja kutoka Hong Kong na Macao wamechukua asilimia takriban 68 ya idadi ya jumla ya abiria, likiwa ni ongezeko la asilimia 25 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 55 linaunganisha Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, mji wa Zhuhai wa Mkoa wa Guangdong, na Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao. Limeleta fursa nyingi za kiuchumi na manufaa kwa Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha