Ecuador yakosolewa vikali kidiplomasia baada ya polisi kuvamia ndani ya ubalozi wa Mexico

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2024

QUITO - Ecuador imekumbana na ukosoaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa za Amerika Kusini siku ya Jumamosi baada ya polisi wake kuvamia ndani ya ubalozi wa Mexico huko Quito na kumkamata Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Jorge Glas, ambaye amekuwa akiishi chini ya hifadhi ya ukimbizi katika ubalozi huo tangu mwezi Desemba mwaka jana.  Ukosoaji wa kidiplomasia  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres "amesikitishwa" na uvamizi uliofanywa na vikosi vya usalama vya Ecuador katika ubalozi wa Mexico huko Quito ili kumkamata Glas anayetuhumiwa kwa ufisadi, amesema Stephane Dujarric, msemaji wa Guterres, siku ya Jumamosi.  Guterres amezitaka Ecuador na Mexico kuonyesha hali ya "upatanishi" na "kusuluhisha tofauti zao kwa njia za amani," msemaji huyo amesema katika taarifa yake.  Tukio hilo limeifanya Mexico kuvunja mara moja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ecuador. "Huu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na mamlaka ya Mexico," Rais Andres Manuel Lopez Obrador ameandika kwenye mtandao wa X, zamani Twitter.  Nchi nyingine za Amerika Kusini, zikiwemo Cuba na Bolivia pamoja na Brazili na Nicaragua, zimeshirikiana kuiunga mkono Mexico kufuatia uvamizi huo.  "Mshikamano wetu wote uko na Mexico, katika kukabiliana na ukiukwaji usiokubalika wa Ubalozi wake huko Quito. Mkataba wa Vienna juu ya Uhusiano wa Kidiplomasia, ambao ni sehemu muhimu ya sheria za kimataifa, lazima uheshimiwe na wote," Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel ameandika kwenye mtandao wa X.  Jorge Glas ni nani? Glas alikuwa Makamu wa Rais wa Ecuador chini ya serikali ya Rais Rafael Correa kuanzia Mwaka 2013 hadi 2017.  Mwaka 2017, alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kuchukua hongo kutoka kwa kampuni moja ya ujenzi ya Brazil. Alikutwa na hatia tena Mwaka 2020 kwa kutumia pesa kutoka kwa wanakandarasi ili kufadhili kampeni za kisiasa za Correa, na kupelekea kuhukumiwa kifungo cha miaka minane jela.  Aliachiliwa huru mara ya mwisho mwezi Novemba 2022, lakini viongozi wa Ecuador hivi majuzi wamemshutumu tena Glas kwa ubadhirifu wa pesa za serikali zilizokusudiwa kwa ajili ya ujenzi mpya baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi la Mwaka 2016. Ecuador, ambayo iliomba idhini ya Mexico kuingia katika ubalozi huo mwezi Machi ili kumkamata Glas, inadai kuwa ombi la Jorge Glas la hifadhi ya ukimbizi lilikuwa kinyume cha sheria na imetaka kumrejeshwa nchini Ecuador.  Kwa mujibu wa Mkataba wa Vienna juu ya Uhusiano wa Kidiplomasia, ambao ni mkataba unaodhibiti uhusiano ya kimataifa, nchi hairuhusiwi kuingilia ubalozi ulioko ndani ya mipaka yake.

Polisi wa Ecuador wakiwa kwenye doria huko Quito, Ecuador, Januari 9, 2024. (Picha na Mateo Armas/Xinhua)

QUITO - Ecuador imekumbana na ukosoaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa za Amerika Kusini siku ya Jumamosi baada ya polisi wake kuvamia ndani ya ubalozi wa Mexico huko Quito na kumkamata Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Jorge Glas, ambaye amekuwa akiishi chini ya hifadhi ya ukimbizi katika ubalozi huo tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Ukosoaji wa kidiplomasia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres "amesikitishwa" na uvamizi uliofanywa na vikosi vya usalama vya Ecuador katika ubalozi wa Mexico huko Quito ili kumkamata Glas anayetuhumiwa kwa ufisadi, amesema Stephane Dujarric, msemaji wa Guterres, siku ya Jumamosi.

Guterres amezitaka Ecuador na Mexico kuonyesha hali ya "upatanishi" na "kusuluhisha tofauti zao kwa njia za amani," msemaji huyo amesema katika taarifa yake.

Tukio hilo limeifanya Mexico kuvunja mara moja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ecuador. "Huu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na mamlaka ya Mexico," Rais Andres Manuel Lopez Obrador ameandika kwenye mtandao wa X, zamani Twitter.

Nchi nyingine za Amerika Kusini, zikiwemo Cuba na Bolivia pamoja na Brazili na Nicaragua, zimeshirikiana kuiunga mkono Mexico kufuatia uvamizi huo.

"Mshikamano wetu wote uko na Mexico, katika kukabiliana na ukiukwaji usiokubalika wa Ubalozi wake huko Quito. Mkataba wa Vienna juu ya Uhusiano wa Kidiplomasia, ambao ni sehemu muhimu ya sheria za kimataifa, lazima uheshimiwe na wote," Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel ameandika kwenye mtandao wa X.

Jorge Glas ni nani?

Glas alikuwa Makamu wa Rais wa Ecuador chini ya serikali ya Rais Rafael Correa kuanzia Mwaka 2013 hadi 2017.

Mwaka 2017, alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kuchukua hongo kutoka kwa kampuni moja ya ujenzi ya Brazil. Alikutwa na hatia tena Mwaka 2020 kwa kutumia pesa kutoka kwa wanakandarasi ili kufadhili kampeni za kisiasa za Correa, na kupelekea kuhukumiwa kifungo cha miaka minane jela.

Aliachiliwa huru mara ya mwisho mwezi Novemba 2022, lakini viongozi wa Ecuador hivi majuzi wamemshutumu tena Glas kwa ubadhirifu wa pesa za serikali zilizokusudiwa kwa ajili ya ujenzi mpya baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi la Mwaka 2016.

Ecuador, ambayo iliomba idhini ya Mexico kuingia katika ubalozi huo mwezi Machi ili kumkamata Glas, inadai kuwa ombi la Jorge Glas la hifadhi ya ukimbizi lilikuwa kinyume cha sheria na imetaka kumrejeshwa nchini Ecuador.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Vienna juu ya Uhusiano wa Kidiplomasia, ambao ni mkataba unaodhibiti uhusiano ya kimataifa, nchi hairuhusiwi kuingilia ubalozi ulioko ndani ya mipaka yake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha