AU yateua mjumbe maalum wa kupambana na mauaji ya kimbari na ukatili wa halaiki barani Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2024

 Picha hii ikionesha Sanaa yenye mada ya kumbukumbu ya miaka 29 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi Mwaka 1994 katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali mjini Kigali, Rwanda, Aprili 7, 2023. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)

Picha hii ikionesha Sanaa yenye mada ya kumbukumbu ya miaka 29 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi Mwaka 1994 katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali mjini Kigali, Rwanda, Aprili 7, 2023. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)

ADDIS ABABA - Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat siku ya Jumamosi amemteua Adama Dieng wa Senegal kuwa mjumbe maalum wa kwanza wa AU wa kuzuia uhalifu wa mauaji ya kimbali na ukatili mwingine wa halaiki.

Faki amesema siku hiyo kwenye mtandao wa X (Twitter) kwamba, Adama Dieng akiwa mjumbe maalum wa kwanza wa umoja huo wa Bara la Afrika wenye nchi wanachama 55 kwa ajili ya kuzuia uhalifu wa mauaji ya kimbari na ukatili mwingine wa halaiki, Dieng atahimiza ajenda ya AU ya kupambana na itikadi ya chuki na mauaji ya kimbari katika Bara la Afrika.

Hapo awali Dieng aliteuliwa na Ban Ki-moon aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Kuzuia Mauaji ya Kimbari.

Umoja wa Mataifa umesema, Adama Dieng akiwa mtaalam wa sheria na haki za binadamu, Dieng ana taaluma iliyotukuka katika kuchangia kwenye uimarishaji wa utawala wa kisheria, kupiga vita upuuzaji wa sheria na kuhimiza ujengaji wa uwezo katika eneo la taasisi za mahakama na za kidemokrasia, ikiwemo kupitia ujumbe mbalimbali wa kufanya uchunguzi, machapisho na vyombo vya habari.

Mshauri Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuia Mauaji ya Kimbari Adama Dieng (Kati, mbele) akihutubia wakati  ulipotolewa kwa Mkakati na Mpango wa Utekelezaji wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kauli za Chuki, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 18, 2019. (Xinhua) /Li Muzi)

Mshauri Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuia Mauaji ya Kimbari Adama Dieng (Kati, mbele) akihutubia wakati ulipotolewa kwa Mkakati na Mpango wa Utekelezaji wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kauli za Chuki, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 18, 2019. (Xinhua/Li Muzi)

Uteuzi huo wa Dieng umekuja wakati AU imeandaa shughuli ya ngazi ya juu siku ya Jumapili ya kukumbuka miaka 30 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari ya Mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda chini ya kaulimbiu ya "Kumbuka-Ungana-Sisitiza".

Tangu Mwaka 2010, AU imekuwa ikiandaa matukio mbalimbali ya kukumbuka mauaji hayo kila mwaka Aprili 7, kwa mujibu wa uamuzi wa viongozi wa Afrika.

AU imesema kuwa, mwaka wa 2024 unaashiria "wakati muhimu wa kuwakumbuka marehemu, kuwaunga mkono walionusurika, na kuungana pamoja ili kuzuia ukatili kama huo kutokea tena."

Imesema shughuli za kumbukumbu ni kama jukwaa muhimu la kuendelea kuamsha uelewa zaidi wa watu wa Afrika na jumuiya ya kimataifa kuhusu thamani ya maisha na utu na kusisitiza ahadi za pamoja za kulinda na kudumisha haki za msingi za binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha