Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na naibu Waziri Mkuu wa Vietnam mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2024

Wang Yi, Mwenyekiti Mwenza wa upande wa China wa Kamati ya Uendeshaji wa Ushirikiano wa pande mbili za China na Vietnam, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Tran Luu Quang ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa kamati hiyo kwa upande wa Vietnam, mjini Beijing, China, Aprili 8, 2024. (Xinhua/Chen Bin)

BEIJING – Wang Yi, Mwenyekiti Mwenza wa upande wa China wa Kamati ya Uendeshaji wa Ushirikiano wa pande mbili za China na Vietnam, amekutana na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Tran Luu Quang ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo kwa upande wa Vietnam, mjini Beijing Jumatatu ambapo amesema kuwa kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Vietnam kunaendana na maslahi ya kimsingi ya nchi na watu wa pande hizo mbili, kunaendana na mwelekeo wa maendeleo na hatua za zama hizi, na kuna umuhimu mkubwa kwa nchi hizo mbili katika kuharakisha ujenzi wa mambo yao ya kisasa na kuendeleza lengo kuu la ujamaa.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema China ingependa kushirikiana na Vietnam katika kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, kutoa mchango kwa kutosha kuratibu jukumu la Kamati ya Uendeshaji wa Ushirikiano wa pande mbili za China na Vietnam, kuzidisha ushirikiano katika nyanja kama vile uchumi, biashara, uwekezaji, muunganisho wa miundombinu, sayansi na teknolojia na uvumbuzi, kuunda maeneo mapya ya ukuzaji uchumi ya ushirikiano, kuimarisha mawasiliano kati ya watu na watu, kudhibiti ipasavyo tofauti, kuongeza uungaji mkono wa umma kwa urafiki mzuri kati ya nchi hizo mbili, na kuendeleza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Vietnam.

Kwa upande wake Tran Luu Quang amesema kuwa uhusiano kati ya Vietnam na China uko katika kiwango bora zaidi katika historia, na kuongeza kuwa Vietnam inapenda kushirikiana na China kuchukua ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya Vietnam na China kama mwongozo, kufanya kwa kutosha jukumu la Kamati hiyo ya Uendeshaji wa ushirikiano kati ya pande mbili, na kuendeleza kwa pamoja lengo kuu la pamoja la ujamaa kwa ajili ya kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha