Kenya yawa katika hali ya tahadhari kukabiliana na matishio ya kigaidi

(CRI Online) April 09, 2024

Serikali ya Kenya jana imesema kuwa vyombo vyake vya usalama viko katika hali ya tahadhari kukabiliana na matishio ya kigaidi kote nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa ya Kenya Raymond Omollo, amesema licha ya matukio machache yaliyoripotiwa katika mpaka wa Kenya na Somalia, nchi hiyo kwa ujumla iko salama.

Kauli yake hiyo imekuja kufuatia ushauri wa tahadhari za kusafiri kwenda Kenya zilizotolewa na Uingereza na Australia wikiendi iliyopita, ambazo zilionya kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi yanayolenga raia wa kigeni nchini Kenya.

Katika kuitikia tahadhari hiyo, polisi wa Kenya wamewahakikishia Wakenya na raia wa kigeni kuwa hakuna haja ya hofu, kwani wamechukua hatua za kukabiliana na matishio hayo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha