Ethiopia yadhamiria kuwa kiongozi wa kikanda wa kampuni zinazoibuka

(CRI Online) April 09, 2024

Serikali ya Ethiopia imetangaza matarajio yake ya kuwa kiongozi wa kikanda kwa kampuni zinazoibuka haswa katika sekta ya uvumbuzi.

Shirika la Habari la Ethiopia (ENA) limeripoti kuwa, Waziri wa Kazi na Ujuzi wa nchi hiyo Muferihat Kamil amesisitiza msimamo wa serikali wa kuunga mkono kampuni hizo, na haja ya kuongeza ushirikiano kati ya taasisi za serikali, sekta binafsi pamoja na washirika wa kimataifa katika kukuza kampuni hizo.

Waziri wa Viwanda wa nchi hiyo Melaku Alebel pia amesisitiza umuhimu wa kimkakati wa kampuni zinazoibuka, haswa zile za sekta ya teknolojia, akisema zitachochea maendeleo ya sekta nyingine.

Kwa mujibu wa Wizara ya Uvumbuzi na Teknolojia ya Ethiopia, nchi hiyo imeshuhudia “ongezeko la kasi” la idadi ya kampuni zinazoibuka katika miaka mitano iliyopita.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha