Rais Xi Jinping akutana na waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2024

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 9, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 9, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING- Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov Jumanne mjini Beijing ambapo amemtaka afikishe salamu za dhati kwa Rais wa Russia Vladimir Putin.

Huku akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya kutimia miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, Rais Xi amesema China na Russia zimeanzisha njia mpya ya kuishi pamoja kwa masikilizano na ya ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi kubwa na majirani, hali ambayo imenufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao na kuchangia hekima na nguvu katika haki na usawa wa kimataifa.

"Mimi na Rais Putin tumekubaliana kuendelea kudumisha mawasiliano ya karibu ili kuhakikisha maendeleo mazuri na ya kasi ya uhusiano kati ya China na Russia. Pande hizo mbili zinapaswa kuchukua fursa ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na Miaka ya Utamaduni ya China na Russia ili kutekeleza kikamilifu makubaliano muhimu yaliyofikiwa na Rais Putin na mimi," amesema.

Rais Xi amesisitiza kuwa, China inaunga mkono watu wa Russia katika kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali yake ya kitaifa, na kuiunga mkono Russia katika kupambana na ugaidi na kudumisha usalama na utulivu wa kijamii.

China daima inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia, na ingependa kuimarisha mawasiliano ya pande mbili na Russia na kuimarisha uratibu wa kimkakati wa pande nyingi katika BRICS na Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai.

Ameongeza kuwa nchi hizo mbili zitaonyesha uwajibikaji zaidi, kuunganisha nchi za Kusini katika moyo wa usawa, uwazi, na ujumuishaji, kuendeleza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa kimataifa, na kuongoza kwa hamasa kubwa ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

Kwa upande wake Lavrov amewasilisha salamu za Rais Putin za kirafiki na kutakia kila la kheri kwa Rais Xi. Amesema, chini ya uongozi madhubuti wa Rais Xi, China imepata mafanikio ambayo yamefuatiliwa na dunia nzima na kutoa fursa muhimu kwa nchi nyingine kupata maendeleo ya pamoja, ambayo Russia inayathamini na kuyapongeza sana.

Lavrov amesema kipaumbele cha sera ya mambo ya nje ya Russia ni kuzidisha na kuboresha kwa pande zote uhusiano kati yake na China, na kuchaguliwa tena kwa Rais Putin kunahakikisha kuendelea kwa uhusiano kati ya Russia na China.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 9, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Aprili 9, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha