China yatangaza hatua za kuendeleza uboreshaji wa vifaa vya viwandani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2024

Picha hii iliyopigwa tarehe 25 Machi 2024 ikinyesha mstari wa kuunganisha sehemu za magari kwenye kiwanda cha magari cha Xiaomi mjini Beijing, China. (Xinhua/Peng Ziyang)

Picha hii iliyopigwa tarehe 25 Machi 2024 ikinyesha mstari wa kuunganisha sehemu za magari kwenye kiwanda cha magari cha Xiaomi mjini Beijing, China. (Xinhua/Peng Ziyang)

Beijing - Serikali ya China imetangaza malengo na hatua maalum za kuboresha vifaa vya viwandani kwa juhudi mpya za kupanua uwekezaji wenye ufanisi zaidi na kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.

Kwa mujibu wa mpango kazi uliotolewa kwa pamoja na idara saba za serikali ya China, ikiwa ni pamoja na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China, nchi hiyo itaongeza uwekezaji wa vifaa vya viwandani kwa asilimia zaidi ya 25 kwa kipindi cha Mwaka 2023-2027.

Hadi kufikia Mwaka 2027, kiwango cha matumizi ya vifaa vya kidijitali vya utafiti na uundaji wa bidhaa (R&D) na zana za kubuni katika kampuni kubwa kitazidi asilimia 90, na asilimia zaidi ya 75 ya michakato yao muhimu ya uzalishaji itadhibitiwa na mashine.

Mpango huo unasema, sekta ya viwanda itapiga hatua katika maendeleo ya teknolojia za hali ya juu, za akili bandia na za kijani, na ujenzi wa mfumo wa kisasa wa viwanda utaharakishwa.

Hasa, kuharakisha kuondoa vifaa vilivyopitwa na wakati katika sekta mbalimbali zikiwemo mashine za kilimo na ujenzi na baiskeli zinazotumia umeme. Kampuni za teknolojia ya hali ya juu katika anga, teknolojia ya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua, betri za nishati na uchachushaji wa kibaolojia zitawezeshwa na kuhamasishwa ili kuendeleza vifaa vya teknolojia ya hali ya juu vyenye ufanisi zaidi na vya kutegemeka zaidi.

Kwa upande wa mageuzi ya kidijitali, uboreshaji wa vifaa katika sekta kama vile zana za mashine zinazodhibitiwa na kidigitali, roboti za viwandani na usambazaji wa bidhaa unaotumia teknolojia za kisasa utahimizwa. Viwanda vinavyotumia teknolojia za akili bandia vitashuhudia maendeleo ya haraka, vikiwa na matumizi ya pande zote ya teknolojia mpya ikiwa ni pamoja na akili bandia, 5G na mifumo ya kompyuta ya teknolojia ya hali ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha