Ubalozi wa China wazitaka Marekani, Uingereza na Australia kuacha kuunda kambi mahsusi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2024

LONDON - Ubalozi wa China nchini Uingereza umepinga kithabiti Marekani, Uingereza na Australia kushikilia kuhimiza kile kinachoitwa uhusiano wa wenzi wa usalama wa pande tatu bila kujali wasiwasi mkubwa wa nchi za kikanda na jumuiya ya kimataifa kuhusu hatari za kuenea kwa nyuklia.

Msemaji wa ubalozi huo ametoa kauli hiyo siku ya Jumanne, wakati akijibu swali kuhusu taarifa ya pamoja ya mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo tatu wakidai kuwa wanafikiria kufanya ushirikiano na Japan katika miradi ya uwezo wa hali ya juu ya AUKUS Pillar II.

Msemaji huyo amesema hatua kama hizo bila shaka zitaongeza hatari ya kuenea kwa nyuklia, kuzidisha mashindano ya silaha katika eneo la Asia-Pasifiki, na kuharibu amani na utulivu wa kikanda. "China inafuatilia zaidi na inapinga kithabiti jambo hili."

"Tunazitaka Marekani, Uingereza na Australia kuacha mawazo ya Vita Baridi, kuacha kuunda kundi la kujitenga, na kuacha kuzusha matatizo na mapambano ya kambi katika eneo la Asia-Pasikifi,"mwanadiplomasia huyo amesema.

"Japan lazima ikumbuke mafunzo kwenye historia na kuwa na busara kuhusu maneno na vitendo vyake linapokuja suala la usalama wa kijeshi" amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha