Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu asema hakuna nguvu inayoweza kuzuia mashambulizi ya ardhini dhidi ya Rafah

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (wa pili kushoto, mbele) akizungumza na wanajeshi katika kambi ya kijeshi nje ya Tel Aviv, Israel, Aprili 9, 2024. (Amos Ben-Gershom/GPO/Xinhua)

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (wa pili kushoto, mbele) akizungumza na wanajeshi katika kambi ya kijeshi nje ya Tel Aviv, Israel, Aprili 9, 2024. (Amos Ben-Gershom/GPO/Xinhua)

JERUSALEM - Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema siku ya Jumanne kwamba Israel itaanzisha mashambulizi ya ardhini dhidi ya Kundi la Hamas katika Mji wa Rafah wa Ukanda wa Gaza na kwamba "hakuna nguvu yeyote duniani" inayoweza kuizuia.

Jeshi la Israel "litateketeza kabisa vikosi vya Hamas, ikiwa ni pamoja na kikosi kilichoko Rafah," Netanyahu amewaambia wanajeshi wapya kujiunga na jeshi katika kambi ya kijeshi nje ya Tel Aviv.

Amesema jumuiya ya kimataifa inajitahidi kuzuia mashambulizi ya ardhini katika mji huo wa Palestina, lakini "hakuna nguvu yeyote duniani ambayo inaweza kutuzuia."

Hata hivyo, Netanyahu hakutaja tarehe maalum ya kuanza kwa mashamulizi hayo.

Umoja wa Mataifa na wataalamu wa masuala ya misaada wamekuwa wakionya mara kwa mara kwamba operesheni yoyote ya kijeshi huko Rafah, mji wa kusini mwa Gaza itasababisha idadi kubwa ya vifo vya raia wa Gaza huku watu takriban milioni 1.4 wamekimbilia huko kutafuta hifadhi kutokana na mashambulizi ya mabomu katika maeneo mengine.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihutubia wanajeshi wapya kujiunga na jeshi katika kambi ya kijeshi nje ya Tel Aviv, Israel, Aprili 9, 2024. (Amos Ben-Gershom/GPO/Xinhua)

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihutubia wanajeshi wapya kujiunga na jeshi katika kambi ya kijeshi nje ya Tel Aviv, Israel, Aprili 9, 2024. (Amos Ben-Gershom/GPO/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha