Baraza la Usalama la UN laanza majadiliano juu ya ombi la Palestina kuwa nchi mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa

(CRI Online) April 10, 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewasilisha ombi la Palestina kuwa nchi mwanachama rasmi wa Umoja huo kwa Kamati ya Uanachama Mpya ya Baraza hilo siku ya Jumatatu, ambapo kwa mujibu wa ratiba, Kamati hiyo imefanya mazungumzo ya ndani kwa mara ya kwanza siku hiyo hiyo.

Palestina kwa sasa ni mjumbe mwangalizi wa Umoja wa Mataifa na ikitaka kuwa mwanachama rasmi wa Umoja huo, inahitaji idhini kutoka kwa Baraza la Usalama na Baraza Kuu la umoja huo.

Mwaka 2011, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas aliwasilisha ombi hilo, lakini Marekani ilisema ni lazima makubaliano yafikiwe kwanza kati ya Palestina na Israel, na kuonya kuwa itatumia haki yake ya kura ya turufu katika Baraza la Usalama, hivyo kuilazimu Palestina kusitisha ombi lake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha